Hii hapa ni Certificate ya Diploma
nilichopokea baada ya kusota kwa muda wa mwaka mzima yote hayo
namshukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kufikia katika hatua hii
muhimu.
Tuesday, December 11, 2012
Graduation Photos
Ilikuwa ni kipindi nahitimu na kupokea Certificate ya Diploma ya
designing & graphics katika Chuo cha Musoma information Center.
Picha hii ya juu nilikuwa napokea cheti zinazofuata niko na wanafunzi
wenzangu pamoja na teacher wetu Eli Munuve katika shamrashamra za shereh
hiyo.
Monday, December 10, 2012
MKURUGENZI WA ABC-Foundation Bw Eustuce Nyarugenda Afariki dunia katika mazingira ya kutatanisha
MSTAHIKI MEYA WA MANSPAA YA MUSOMA ALEX KISURURA AONGOZA MAELFU KATIKA KUUGA MWILI WA MWANAHARAKATI WA KUTETEA HAKI ZA BINADAMU PAMOJA NA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO EUSTUCE NYARUGENDA NYUMBANI KWAKE LEO MCHANA
MWILI WA MAREHEMU NYARUGENDA UKIINGIZWA NYUMBANI KWAKE MAENEO YA KIGERA BONDENI |
MMOJA WA STAFF WA SHIRIKA LA ABC FOUNDATION MR KURWA AKIZUNGUMZA NAMNA WALIVYOFANYA KAZI NA NYARUGENDA |
BAADHI YA WAOMBOLEZAJI WAKIWA MSIBANI |
MWILI WA NYARUGENDA UMEHIFADHIWA HUMU |
UKIFUNULIWA KWA AJILI YA WAOMBOLEZAJI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO |
KAPUMZIKE KWA AMANI KOMLEDI NYARUGENDA |
STAFF WA ABC FOUNDATION MARIA ALIPOSHINDWA KUJIZUIA. |
MRATIBU WA SHIRIKA LA MARA DEVELOPMENT FORUM ALIKUWA NI MMOJA WA WAOMBOLEZAJI |
MSTAHIKI MEYA KISURURA AKITOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO |
MJANE WA MAREHEMU PAMOJA NA WATOTO WAKE WAWILI |
NENO LA MUNGU PIA LILIHUBIRIWA MAHALA HAPA |
SAFARI YA KUELEKEA KARAGWE MKOANI KAGERA KWA AJILI YA MAZISHI |
Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.
MAPATO |
SHILINGI MILIONI
|
||
A | Mapato ya ndani |
11,889,078
|
|
i)mapato ya kodi (TRA) |
10,232,539
|
||
ii)Mapato yasiyo ya kodi |
1,163,533
|
||
B | Mapato ya Halmashauri |
493,006
|
Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.
Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
Zitto akiwasilisha hotuba ya bajeti kivuli
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI NDUGU KABWE
ZUBERI ZITTO (MB), WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI, KUHUSU MAPENDEKEZO YA
MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI NDUGU KABWEZUBERI ZITTO (MB), WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI, KUHUSU MAPENDEKEZO YAMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA2012/2013 ______________________ I. UTANGULIZIMheshimiwa Spika
, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, ninatoa maoni ya Kambiya Upinzani kuhusu Bajeti ya Nchi ya mwaka wa fedha 2012/2013 kwa mujibuwa Kanuni za Bunge Kifungu cha 99(7) toleo la Mwaka 2007.
Mheshimiwa Spika,
Natoa pongezi za dhati kabisa kwa Ndugu WilliamAugustao Mgimwa, Mbunge wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa kwa kuteuliwana Rais kuwa Waziri wa Fedha na Uchumi. Vile vile nawapongeza Ndugu SaadaMkuya na Ndugu Janeth Mbene kwa kuteuliwa kwao kuwa Wabunge nabaadaye kuwa Manaibu Mawaziri katika Wizara hii nyeti sana. Ninawapa polepia maana Wizara ya Fedha sio Wizara lelemama. Kambi ya Upinzaniitaendelea kuisimamia Wizara hii kwa ukaribu sana kama ilivyofanya katikakipindi cha miaka miwili iliyopita. Mtakapofanya vizuri tutawapongeza ilimuongeze juhudi, mtakapoharibu tutawawajibisha.
Mheshimiwa Spika,
Ni dhahiri kwamba Mwaka wa Fedha uliopita ulikuwamwaka mgumu sana kwa Watanzania. Ni mwaka ambao gharama za maishazilipanda kwa kasi kubwa sana na juhudi za Serikali kuwakwamua wananchi nahasa wananchi wanyonge kutoka kwenye lindi la ufukara ziligonga mwamba.Kambi ya Upinzani inawapa pole Watanzania kwani hili ndilo walilochagua.
Muhimu ni kuvumilia mpaka uchaguzi ujao na kufanya mabadiliko ya Serikali ilikuweka Serikali itakayoongozwa na CHADEMA na itakayoweza kukabilichangamoto za sasa na za baadaye.
Mheshimiwa Spika
, naomba tufanye mapitio kidogo ya Bajeti inayomalizamuda wake.
1.
UTEKELEZAJI WA BAJETI ILIYOPITAMheshimiwa Spika
, kabla ya kutoa bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani nivema kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya Serikali iliyopita ili kuona nikwa namna gani Serikali inathamini fedha za walipa kodi, na dhamira yake yakuleta maendeleo ya kiuchumi katika Taifa. Katika kufanya hivyo, tutapitiabaadhi ya maeneo ambayo Kambi ya Upinzani tunaona kuwahayakutekelezwa katika bajeti iliyopita.
Kupunguza Makali ya MaishaMheshimiwa Spika,
Katika Bajeti ya mwaka 2011/12 Serikali ilitangaza nia yakeya kupunguza makali ya maisha. Hatua mbali mbali zilichukuliwa ikiwamokupunguza kodi na tozo kwenye mafuta ya Dizeli na Petroli, kuanza kutekelezampango wa dharura wa umeme na kutoa fedha za kununua chakula kwaWakala wa Chakula. Serikali ilitumia shilingi bilioni 296 na dola za Marekanimilioni 183 kwenye Umeme. Vilevile Serikali ilitumia shilingi bilioni 27 kununuaMahindi na kusambaza kwenye masoko.
Mheshimiwa Spika,
licha ya hatua hizo zilizochukuliwa Mfumuko wa Beiuliongezeka maradufu kutoka wastani wa asilimia 6.3 mwaka 2010/11 mpakawastani wa asilimia 17.8 mwaka 2011/12. Serikali imefeli katika lengo lake lakupunguza makali ya maisha kwa wananchi. Sio tu kwamba Serikali imeshindwakudhibiti upandaji holela wa gharama za maisha bali pia hatua za Serikalizimeongeza kasi ya kupanda kwa makali ya maisha.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani Bungeni katika Hotuba yake mbadala yamwaka 2011/12 iliitaka Serikali kushughulikia msingi wa mfumuko wa Bei hapanchini ambao ni uzalishaji mdogo wa mazao ya chakula. Tumeelezwa na WaziriKivuli wa Mipango na Uchumi kwamba Chakula peke yake ni asilimia 48 yakapu la bidhaa na huduma ambazo mwanachi anatumia. Mfumuko wa Bei yaChakula kinacholiwa nyumbani na kwenye migahawa ilikuwa asilimia 25 mweziAprili 2012 (BoT monthly Economic Review, May 2012). Vile vile mfumuko wa beiwa nishati inayotumika nyumbani na mafuta ya Dizeli na Petroli ulifikia asilimia 25pia mwezi Mei mwaka 2012. Ni dhahiri kwamba iwapo tutadhibiti mfumuko wabei ya chakula tutaweza kushusha mfumuko wa bei kurudi kwenye tarakimumoja.
Mheshimiwa Spika
, Serikali inapendekeza hatua zilezile ilizofanya mwaka wafedha unaokwisha kwa kutoa vibali kwa Wafanyabiashara vya kuagiza Mchelena Sukari. Katika h
otuba yake Waziri wa Fedha anasema ‘…
.
Serikali ilitoa vibalivya kuagiza sukari bila kutoza ushuru wa forodha kiasi cha tani 200,000 ili
kukabiliana na uhaba na kupanda kwa bei ya Sukari…’
(uk 9 ibara ya 15).Baada ya hatua hii bei ya Sukari ilipanda kutoka tshs 1700 mpaka tshs 2800kwenye maeneo mengi nchini. Waziri wa Fedha katika hotuba yake anatoasuluhisho
. Ninanukuu. ‘…hatua za haraka ambazo Serikali itachukua ni pamoja
na kutoa vibali vya uagizaji wa Sukari na mchele kutoka nje….’! Serikali
inachukua hatua zilezile kwa tatizo lile lile ikitegemea matokeo tofauti.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani Bungeni inarejea pendekezo lake lamwaka jana kwa Serikali kutoa vivutio kwa wakulima wadogo kuzalisha chakulakwa wingi. Miongoni mwa vivutio hivyo ni:i.
Kuwekeza kwenye barabara za vijijini ili mazao yao yafike kwenyemasoko na kupata bei nzuri,ii.
Kuwekeza kwenye Usambazaji wa Maji vijijini ili kina mama wasitembeemwendo mrefu kutafuta maji na hivyo kutumia muda mwingi kwenyeuzalishaji,iii.
Kuwekeza kwenye Umeme vijijini ili wafanyabiashara wa vijijini waongezethamani ya mazao. Kwa mfano, kuuza Unga badala ya Mahindi.iv.
Kuwekeza kwenye miundombinu ya Umwagiliaji vijijini ili wakulimawazalishe muda wote wa mwaka.v.
Kuwekeza kwenye Elimu vijijini na pia Afya vijijini ili wananchi wetu wawena Afya bora na waelimike katika mbinu za uzalishaji bora.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani inaamini kuwa, hakuna mbadala wakudhibiti mfumuko wa bei zaidi ya kuongeza uzalishaji wa chakula na kuwekezakwa wananchi wetu. Serikali inafikiria uzalishaji utaongezeka kwa kusaidiawakulima wakubwa ambao watageuza wananchi wetu kuwa Manamba navibarua ndani ya nchi yao. Tuwekeze kwa watu wetu vijijini ili waongezeuzalishaji na kwa kufanya hivyo mfumuko wa Bei ya chakula utakuwa historia.Hakuna mwarobaini wa kupanda kwa bei za vyakula isipokuwa Kilimo.
Mhesimiwa Spika
, Tunatambua kuwa hatua tunazotaka Serikali ifanye ni zamuda wa kati. Kwa muda mfupi tunataka Bodi ya Mazao mchanganyiko,Wakala wa Hifadhi ya Chakula na Bodi ya Sukari zipewe fedha kuagiza Mchelena Sukari na pia kununua kutoka kwa wakulima na kusagisha Mahindi.Wafanyabiashara waagizaji wa Chakula washindane na Taasisi hizi za Ummabadala ya kuwapa vibali ambavyo hutolewa kwa rushwa na hivyo kuongezabei za bidhaa hizo.
Kuwezesha Wananchi Kiuchumi na Kuongeza Ajira.Mheshimiwa Spika,
Serikali imesema kwamba ilichukua hatua mbalimbalikukabiliana na tatizo la Ajira kwa kuongeza fursa za ajira. Miongoni mwa hatuazilizochukuliwa ni pamoja na kuongeza mitaji katika Benki ya Rasilimali, Benki yaWanawake, Benki ya Posta na Twiga Bancorp. Pia Serikali imetangaza kwambaimeajiri walimu, maafisa ugani na watumishi wa Afya. Hatua kama hizi piazimetangazwa kwa mwaka wa Fedha wa 2012/13 ambapo pia Serikaliimetangaza kuajiri watumishi 71,756.
Mheshimiwa Spika
, Duniani kote Serikali haizalishi ajira bali ajira huzalishwa naUchumi mzima ambapo Serikali ni sehemu tu ya Uchumi
(Jobs are created bythe economy
). Takwimu zinaonyesha kwamba kila mwaka Tanzania inaingizakwenye soko la Ajira watu takribani laki saba. Shughuli za Uchumi zikiongezekandio Ajira zinatengenezwa. Serikali inafikiria nini kuhusu vijana takribani milioninane walio shule za Msingi hivi sasa, Vijana milioni 1.7 walio katika Shule zaSekondari hivi sasa, Vijana 200,000 waliopo vyuo vya Ufundi na Wanachuo180,000 walio katika Vyuo vya Elimu ya Juu (takwimu kutoka kitabu cha hali ya
uchumi, 2012 sura ya 19). Serikali ambayo bado inategemea takwimu za Ajiraza Mwaka 2006 inajitamba kwa kuajiri watu 70,000.
Mheshimiwa Spika
, Jukumu la Serikali ni kujenga mazingira ya wananchi kupataajira ama kwa kujiajiri au kwa kuajiriwa na shughuli za uchumi. Lakini ukweli nikwamba Serikali imeshindwa kushughulikia tatizo la Ajira na hasa ajira kwavijana. Tatizo la Ajira kwa Vijana ni Bomu litakalokuja kutulipukia vibaya sanakama hatutakuwa makini nalo. Hii ni nchi ya Vijana. Kutoshughulikia masualayao ni kutoshughulikia masuala ya nchi.
Mheshimiwa Spika
, changamoto ya ajira kwa vijana Bajeti mbadala imeiwekeamikakati mipana ya kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa ya Ummaitakayomeza vijana waliopo mtaani na kuanzisha kwa makusudi na kwa kasiVyuo vya Ufundi stadi na Vyuo vya Ufundi na Mafunzo vingi. Kambi ya UpinzaniBungeni inapendekeza Uwekezaji wa Miundombinu Vijijini kama njia yakupunguza tatizo la ajira kwa vijana. Vilevile tunapendekeza Miradi mikubwa yakuongeza mazao ya Kilimo hasa Pamba, Korosho na Katani ili kupanua Ajira.Kambi ya Upinzani pia inapendekeza kujenga VETA katika kila Halmashauri yaWilaya na Chuo cha Ufundi katika kila Mkoa ili kutoa ujuzi kwa vijana ili wawezekukabili maisha yao. Badala ya Serikali kukopa kwa ajili ya Matumizi ya kawaida,Serikali ikope kujenga Vyuo vya Ufundi Stadi na vyuo vya Ufundi na Mafunzo. NiLazima viongozi sio tu tuwe makini bali tuonekane kuwa makinitunaposhughulikia suala la Ajira kwa Vijana.
Sera ya MapatoMheshimiwa Spika,
Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza vipaumbele katikasera ya Mapato ambavyo ni pamoja na kukusanya Mapato ya Serikali mpakazaidi ya asilimia 20 ya Pato la Taifa ili kuwezesha kujitegemea kupata fedha zamiradi ya maendeleo. Pia Kambi ya Upinzani inakusudia kufanya marekebishombalimbali ya sheria za kodi ili kulinda viwanda vya ndani vinavyotumiamalighafi za kilimo na mifugo za hapa nchini, kupanua wigo wa Mapato kwakutunga sheria ya kulazimu kila Mtanzania kujaza fomu za marejesho ya kodi nakurekebisha viwango vya kodi ya Mapato (PAYE). Vile vile tunapendekezakufanya marekebisho ya sheria za kodi kwenye sekta za madini na mawasilianoili kuongeza mapato ya Serikali.
Mheshimiwa Spika
, katika mwaka wa Fedha 2011/12 Serikali ilichukua hatuambalimbali katika masuala ya Kodi. Katika Bajeti mbadala pia tulipendekezahatua mbali mbali ambazo tuliona zitaongeza mapato ya Serikali na hivyokutuwezesha kuendeleza nchi yetu. Baadhi ya hatua mbalimbalitulizopendekeza Serikali imetangaza kuzitekeleza.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani katika Bajeti Mbadala ya mwaka 2011/12ilipendekeza masuala yafutayo ili kuongeza mapato ya Serikali.1.
Hatua zifuatazo zilipendekezwa ili kuweza kukabiliana na ukwepaji wakodi unaofanywa na makampuni makubwa ya kimataifa (MultinationalCorporations) na hatimaye kulipunguzia taifa mapato:
Kutunga sheria kwa kuimarisha zaidi sheria ya Kodi ya Mapato yamwaka 2004 kwamba, mikopo ya makampuni kwenye uwekezaji,kwa sababu za kikodi, isizidi asilimia 70 ya mtaji wote uliowekezwana hii ianze mara moja bila kujali mikataba iliyopo.(ii)
Kutunga sheria kuhakikisha kwamba riba kwenye mikopo kutokaMakampuni yanayohusiana (sister companies) haitaondolewakwenye kutoza kodi (not tax deductible).(iii)
Kuhakikisha kwamba mauziano ya Kampuni yoyote ambayo malizake zipo Tanzania yanatozwa kodi ya asilimia 30% kama
‘ongezeko la mtaji’ (‘capital gains’
).
Mheshimiwa Spika
, katika mapendezo haya ni pendekezo moja tu ndilolimechukuliwa na Serikali katika Bajeti ya mwaka 2012/13 nalo ni pendekezo la
‘capital gains tax’
. Hata hivyo Pendekezo la Serikali lina makosa makubwa sanaya kifundi. Waziri wa Fedha Mhe.
Mgimwa amesema, ninanukuu ‘
Kuanzisha kodiitokanayo na uuzaji wa rasilimali ya uwekezaji (capital gains tax) kwenye uuzaji
wa HISA za kampuni mama ya nje ya nchi’
Mheshimiwa Spika
, Ukisoma pendekezo letu kwa haraka utaona kama Serikaliimelichukua lilivyo, lakini kwa jicho la kiuchumi pendekezo la Serikali na lile laKambi ya Upinzani ni mambo tofauti sana. Pendekezo la Serikali linazungumziaHISA. Mamlaka ya Mapato Tanzania haitakuwa na mamlaka (jurisdiction to tax)kutoza kodi kwa Kampuni mama (as a source or even residence). Mamlaka yaMapato Tanzania ina mamlaka na Mali (assets) zilizopo Tanzania za Kampunimama. Kwa mfano, wakati kampuni ya Barrick inanunua mgodi wa Bulyanhuluhaikuinunua Kampuni ya Kahama mining ltd bali ilinunua hisa zote za Kampuniya Sutton Resources. Vile vile, wakati Zain inanunua Celtel, haikununua Celtel
Tanzania ltd bali Celtel Africa BV ambayo ilikuwa inamiliki Celtel Tanzania BVambayo ilimiliki Celtel Tanzania ltd. Hivyo hivyo ilikuwa kwa AirTel ilipoinunuaZain.
Kukwepa mitego hii ya Mashirika ya Kimataifa (MNCs) sheria itajekwamba Kodi hii itozwe kwa Mali zilizopo Tanzania na sio kwa HISA kamaalivyopendekeza Waziri wa Fedha
. Hata hivyo Kambi ya Upinzani inatambuahatua hiyo ya Serikali kuchukua wazo hili ili kuongeza Mapato ya nchi.
Misamaha ya KodiMheshimiwa Spika,
Katika Bajeti ya mwaka 2011/12 Serikali iliahidi kupunguzamisamaha ya Kodi mpaka kufikia asilimia 1 ya Pato la Taifa. Ahadi hiihaikutekelezwa na Serikali na badala yake imerejea kuahidi tena. Waziri wa
Fedha ameliambia Bunge katika hotuba yake, nanukuu ‘
kuendelea kufanyamapitio ya sharia mbalimbali zinazotoa misamaha ya kodi kwa lengo lakudhibiti na kupung
uza misamaha hiyo’
(uk.39). Badala ya Serikali kutuambiahivi sasa misamaha ya kodi imefikia asilimia ngapi, imeendelea kutoa ahadiisizoweza kutekeleza.
Mheshimiwa Spika,
Katika Taarifa ya Utafiti uliofanywa na Jopo la Taasisi za dinihapa nchini waliyo
iita ‘
The One Billion Dollar Question’
imeonekana kwambaTanzania inapoteza takribani shilingi trilioni 1.7 kutokana na misamaha ya kodi,ukwepaji wa kodi, utoroshaji wa mitaji nje na udanganyifu katika biashara yakimataifa. Fedha hizi ni zaidi ya jumla ya Bajeti za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naNishati na Madini. Fedha hizi ni zaidi ya Mkopo ambao Serikali itadhamini kwaTPDC ili kujenga Bomba la Gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam. Fedhahizi zinazopotea kutokana na misamaha ya kodi ni zaidi ya gharama za Ujenziwa Gati mpya katika Bandari ya Dar es Salaam. Kambi ya Upinzaniinawapongeza Viongozi wa Dini kwa kufanya kazi hii nyeti sana lakini
tunampongeza zaidi Mtafiti Mtanzania Dokta Prosper Ngowi kwa kushiriki katikautafiti huu. Tunaishauri Serikali kusoma Taarifa hii na kutekeleza mapendekezoyake ili kuongeza mapato ya Serikali. Lugha za kufanya mapitio kila mwakahazisaidii, wananchi wanataka kuona misamaha ya kodi imepungua mpakakiwango kinachostahili cha asilimia 1 ya Pato la Taifa.
Kurekebisha mfumo wa Kodi ya MapatoMheshimiwa Spika
, Bajeti mbadala ya mwaka 2011/12 ilipendekeza kuifanyiamarekebisho sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004. Tunarejea pendekezoletu na kuongeza pia kwamba sehemu ya kodi ya Mapato inayotoa fursa(grandfathering) kwa Kampuni za Madini kutumia sheria ya kodi ya Mapatoiliyofutwa ya mwaka 1973, ifutwe. Pendekezo letu lina lengo la kutaka kuweka
mfumo wa ‘straightline method of depreciation’ ya asilimia 20 badala ya sasaambapo Kampuni za Madini hufanya ‘100% depreciation’ kwenye Mitamboyao mwaka wa kwanza na hivyo kuchelewesha kulipa ‘Corporate Tax’.
Mheshimiwa Spika
, Serikali imeamua kupandisha kiwango cha chini cha kipatoili kutoza kodi ya Mapato (PAYE) kutoka tshs 135,000 mpaka tshs 170,000 bilakushusha kodi yenyewe. Hii haitamsaidia mwananchi hata kidogo kwani badokiwango cha kodi cha asilimia 14 kipo juu sana. Vile vile kiwango cha chini chapato litakalotozwa kodi kitawaathiri wafanyakazi wa Serikali maana ndioambao Serikali ina mamlaka ya kutangaza kima cha chini cha Mshahara waona kuwaacha wafanyakazi wa Sekta Binafsi ambao wengi hulipwa kiwangokidogo sana cha mishahara. Kimsingi kutokana na tangazo lake, Waziri waFedha ametangaza kima kipya cha chini cha mshahara kuwa kitakua tshs170,000.
Mheshimiwa Spika
, tunarejea kauli yetu kwamba kupanda kwa gharama zamaisha kumepunguza uwezo wa matumizi ya wananchi walioajiriwa na kulipwamishahara ambayo inakatwa kodi (PAYE). Tunapendekeza kwamba PAYE ianzieasilimia 9 kutoka asilimia 14 na kiwango cha chini cha kutoza kiwe tshs 150,000.Tunatambua kuwa kodi hii ni chanzo kikubwa cha Mapato kwa Serikali ambapokwa mwaka huu wa Fedha kinatarajiwa kuingiza takribani shilingi bilioni 1,437(asilimia 18 ya Mapato yote ya kodi yanayokusanywa na TRA) kutoka Idara yaKodi za Ndani (Wafanyakazi wa Serikali tshs 115bn, Wafanyakazi wa Mashirikaya Umma tshs 47bn na Wafanyakazi wa Sekta binafsi tshs 312bn) na Idara yaWalipa kodi wakubwa (Wafanyakazi wa Serikali tshs 450bn, Wafanyakazi waMashirika ya Umma Tshs108bn na Wafanyakazi wa Sekta Binafsi tshs 406bn).Hata hivyo wananchi wanapobakia na pesa za matumizi kodi nyingine kamaVAT na Ushuru wa Bidhaa huongezeka na hivyo kupunguza kiwango chaMapato ya Serikali ambayo yangepotea kutokana na uamuzi huu.
Mheshimiwa Spika
, Hata hivyo bado
kuna haja ya kuangalia upya ‘
taxbrackets
’
na kuzirahisisha kwa kuzipunguza na kuongeza kiwango cha kodi yaMapato kwa watu wenye kipato kikubwa zaidi.
Mheshimiwa Spika
, ili kuongeza mapato kutoka kwa watu wenye kipatokikubwa kambi ya Upinzani inapendekeza mabadiliko katika viwango vya juuvya kodi ya Mapato ambapo tunapendekeza kupandisha kiwango cha juukabisa cha kukokotoa kodi ya mapato (PAYE) kiwe shilingi milioni kumi na kodiiwe asilimia 42 kutoka asilimia 30 ya sasa.
Mheshimiwa Spika
, Tunapendekeza kwamba mtu yeyote anayepata mapatoya zaidi ya shilingi 10,000,000 alipe kodi ya Mapato ya shilingi 500,000 kujumlishana asilimia 42 ya tofauti ya shilingi 10,000,000 na shilingi 3,200,000 kama
inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini. Lengo la mapendekezo haya nikuwafanya watu wenye kipato kikubwa walipe kodi zaidi kulingana na kipatowanachopata maana hivi sasa masikini wanalipa kodi nyingi zaidi kuliko wenyenacho.
Mapato ya kutozwa kodi kwamweziKodi (PAYE) Mapendekezo ya mapato yakutozwa kodi kwa mweziKiwango kipya chaKodi (PAYE)
Mapato yanayozidi shilingi720,000Sh. 112,500 ongeza 30%ya kiasi kinachozidi sh.720,000Mapato yanayozidi 720,000lakini hayazidi sh. 3,199,199Sh.112,500 ongeza 30%ya ziada ya sh. 720,000Mapato yanayozidi sh.3,200,000 lakini hayazidish.9,999,999Sh.190,000 ongeza 38%ya ziada ya 3,200,000.Mapato kuanzia sh. 10,000,000na kuendeleaSh. 500,000 ongeza 42%ya mapato yake.
Mheshimiwa Spika
, Mapendekezo haya hayatapunguza Mapato ya Serikalikwani wigo wa kodi utakuwa umeongezeka kwa kuwagusa wafanyakazi katikasekta binafsi na pia kupata kodi zaidi kutoka kwa watu wenye kipato kikubwazaidi.
Mheshimiwa Spika
, vile vile Kambi ya Upinzani inaendelea kupendekeza kuwamchakato uanze ili
kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi aweanajaza fomu za kodi (tax returns)
kila mwaka. Suala hili ni muhimu sana nalitangazwe mwaka huu ili tuwe na mwaka mzima wa kujitayarisha ili lianzeMwezi Julai mwaka 2013. Mtanzania yeyote, awe na kipato au asiwe na kipatoajaze Tax Returns. Mfumo huu utatoa takwimu muhimu sana kwa Mamlaka yaMapato Tanzania na utasaidia sana hapo baadaye kupanua wigo wa Mapato.
Tunapendekeza marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Mapato ili mfumo huuuwepo kisheria ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa.
Mheshimiwa Spika
, Vile vile, Kambi ya Upinzani inapendekeza kuanzishwa kwa
Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita
nakwamba kila mwenye nyumba ya kupangisha lazima atambuliwe na kulipa kodiinavyostahili. Lengo ni kuhakikisha Sekta ya Nyumba inatoa mapato ya kutoshakwa Serikali na kuzuia mianya ya ukwepaji kodi inayofanywa na wenyenyumba.
Presumptive TaxMheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani
Bungeni ilipendekeza mwaka 2011/12kwamba ushauri wa Mradi wa kuboresha mfumo wa kodi (Tax ModernisationProject) ambao ulishauri kwamba ipo haja ya kuainisha Kodi ya VAT naPresumptive Tax, utekelezwe. Tunashauri kuwa kodi anayotozwamfanyabiashara ndogondogo kabla hajaanza kufanya biashara ifutwe kabisa.Uamuzi huu utapunguza mapato ya Serikali (Shilingi bilioni 21.6 kwa mujibu waKitabu cha Bajeti Vol. I) katika kipindi cha muda mfupi lakini itakuwa ni chanzokikubwa sana cha mapato katika kipindi cha muda mrefu.
Vyanzo vipya vya MapatoMheshimiwa Spika
,
Pamoja na kupitia vyanzo vya mwaka jana na kulinganishana mapendekezo ya Serikali, Kambi ya Upinzani bado inapendekeza vyanzovya ziada mwaka huu ili kuboresha Mapato ya Serikali.
Kupanua wigo wa Skills Development levyMheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani tunapenda kushukuru kuwa wazo letu lakutoza kodi ya
skills development levy
tuliyopendekeza katika hotuba yetu yamwaka uliopita lilifanyiwa kazi na serikali lakini kwa mwaka ujao wa fedhatunaitaka serikali kuipitia upya kodi kwa kuongeza wigo wa wachangiaji ili kuwana fedha za kutosha kwa ajili ya kugharamia elimu ya juu.
Mheshimiwa Spika
, tunapendekeza kiwango cha tozo ya kuendeleza stadi (
skillsdevelopment levy
–
SDL)
kishuke kutoka asilimia 6 ya sasa mpaka asilimia 4.Tunapendekeza kuwa Waajiri wote walipe kodi hii ikiwemo Serikali na Mashirikaya Umma. Lengo ni kupunguza mzigo kwa Waajiri na kuondoa ubaguzi kwaniwanaofaidika na tozo hii (wanafunzi wa elimu ya Juu) pia huajiriwa na Serikalina Mashirika ya Umma. Serikali ilipanga kukusanya tshs 161bn kutoka katika tozohii kwa mfumo wa sasa.
Mheshimiwa Spika
, Marekebisho ambayo Kambi ya Upinzani inayapendekezayataongeza mapato ya Serikali mpaka tshs 320bn.
Mheshimiwa Spika
, Waziri wa Fedha katika tozo hii amesema Serikali ‘itapitiaupya maudhui ya viwango vya tozo’ hii. Kambi ya Upinzani imetamka maudhui
na viwango na tunaiomba Serikali itekeleze pendekezo hili.
Mheshimiwa Spika
, Tunapendekeza mgawanyo wa tozo hii urekebishwe kwakuongeza mapato yatakayokwenda kwenye Vyuo vya Ufundi mchundo.
Mheshimiwa Spika
, kama wanafunzi wetu watasomeshwa na kodi hii basituangalie upya mfumo wa Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu. Fedha
inayopatikana kwenye Kodi hii itumike kusomesha kwa ‘grant’ wanafunzi
wanaofanya vizuri zaidi darasani na kuwapunguzia mzigo wa mikopo. Vile vile
tuangalie kama tunaweza kukopesha wanafunzi malazi na chakula tu na kutoabure ada na mafunzo kwa vitendo pamoja na vitabu.
Kulinda kazi za WasaniiMheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani mara kwa mara tumekuwa tukieleza jinsiwasanii wanavyoshindwa kunufaika na kazi zao kutokana na kukosekanamfumo rasmi wa kiserikali unaozuia wizi wa kazi za wasanii. Pamoja na serikalikukubali kuahidi kuwa na mfumo rasmi wa kuzuia wizi wa kazi hizo, serikalihaijaweka wazi mfumo rasmi utakaokuwa unatumika kuzuia wizi huo nahatimaye wasanii kunufaika na kazi zao.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya upinzani katika hotuba ya Wizara ya Habari Vijanana Michezo kwa mwaka uliopita tulingumzia suala hili na tulishauri kwambakuwe na utaratibu wa kuweka
sticker
maalumu zinazotolewa na mamlaka zaserikali kuonyesha uhalali wa muuzaji wa kazi za wasanii. Serikali imetekelezapendekezo letu. Hata hivyo tuna maoni tofauti kuhusu namna ya kutekelezapendekezo hili.
Mheshimiwa Spika
, kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, serikali mwaka 2006kupitia gazeti la Serikali Na. 18 la tarehe 10 Mwezi wa Februari, ilianzishautaratibu wa HAKIGRAM kama stiker maalumu za kazi halali za wasaniizinazotolewa na COSOTA. Kambi ya Upinzani tunapendekeza utaratibu huouendelee na Mamlaka ya Mapato TRA ihusike kukusanya mapato kwa ajili yakazi hiyo na COSOTA wataratibu utoaji wa HAKIGRAM. Hii itaenda sambasambana kuzuia uchakachuaji wa HAKIGRAM hizo ili kutopoteza lengo la kuwekamfumo huo. Stiker zisitolewe na TRA bali zitolewe na COSOTA na TRA isimamie
eneo la Mapato tu. Hii itasaidia kwani stiker hizi hazitatumika kupata mapatopeke yake bali pia kuweka kumbukumbu muhimu za kazi za wasanii.
Mapato kutoka Sekta ndogo ya Mawasiliano ya SimuMheshimiwa Spika,
serikali imekuja na pendekezo la kuendelea na kutozaushuru wa bidhaa kwenye masuala ya huduma ya mawasiliano ya simu, jamboambalo litamgusa mtumiaji wa huduma hiyo ambaye ni mwananchi wakawaida na hivyo kuongeza gharama za simu. Kambi ya Upinzani inapingakabisa kuongeza ushuru wa bidhaa kwenye muda wa Maongezi (airtime)kwenye simu za mkononi.
Mheshimiwa Spika
, Hoja ya wananchi hapa ni kwamba Kampuni za Simu zamkononi hazilipi kodi ya kutosha na hasa kodi ya Makampuni (corporate tax).Waziri Mkuu alipokuwa anafunga Bunge la Bajeti mwaka 2011 alitangazaKampuni ambazo ni walipa kodi wakubwa katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.Katika orodha hiyo kulikuwa na Kampuni moja tu ya Simu za Mkononi (Kampuniya AirTel).
Mheshimiwa Spika
, wakati wananchi wanataka kodi zaidi kutoka Kampuni zasimu, Serikali inapendekeza kuongeza kodi kwa mwananchi anayetumia simu.Kampuni zilipe kodi ya Mapato na sio kukandamiza wateja kwa ushuru wabidhaa ilihali huduma zenyewe za simu hazina ubora.
Mheshimiwa Spika
, vilevile wananchi wanalalamika kwamba Kampuni za simuza Mkononi hajiweki wazi mapato yake yote hali iliyopelekea Kamati ya Bungeya POAC kuiagiza TCRA kufunga mtambo utakaoweza kuijulisha TCRA mapatoyote ambayo kampuni za Simu zinapata. Serikali ya Ghana ilifanya hivi nakupandisha maradufu mapato yanayotokana na sekta ndogo ya simu. Hivi sasaGhana, nchi yenye watumiaji wa simu milioni 17 ukilinganisha na Tanzaniayenye watumiaji 23 milioni, inakusanya asilimia 10 ya Mapato ya Serikali kutokakwenye kampuni za Simu peke yake. Iwapo Tanzania ikifikia kiwango cha
Ghana cha asilimia 10 ya Mapato ya ndani ya Serikali kutoka kwenye kampuniza simu, Tanzania itaweza kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 860 kutoka kwenyesekta ndogo ya simu peke yake. Hata hivyo mazingira ya Ghana na Tanzania nitofauti na hivyo tunapendekeza kiwango kutokana na hali yetu.
Mheshimiwa Spika,
Shirika la TCRA kupitia zabuni nambari AE-020/2010-11/C/04imetangaza
‘request for expression of interest for des
ign, development,installation and Management of Telecommunication monitoring system under
build, operate and transfer’
ili kupata chombo cha kufuatilia Mapato yaKampuni za Simu. Kwa mujibu wa ratiba zilizotangazwa na TCRA chombokitakuwa kimeanza kazi mwishoni mwaka huu wa 2012. Kwa dhati kabisanapenda kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA na watumishi wote kwakutekeleza maelekezo ya Kamati ya Bunge kwa haraka ili kuhakikisha mapatokwa nchi yetu.
Mheshimiwa Spika,
kilichotushangaza ni kwamba Waziri wa Fedha na Uchumihakugusia kabisa suala hili muhimu sana kwa mapato ya Serikali badala yakeSerikali imekimbilia kukandamiza wanyonge watumiaji wa Simu na kuyaachaMakampuni ya Simu yakilipa kiduchu kutoka kwenye mapato yao.
Mheshimiwa Spika,
uamuzi huu wa kufuatilia mapato ya Kampuni za Simu naMarekebisho tunayopendekeza ya kujenga uwezo zaidi wa TCRA kwa kuwa na
Idara ya ‘Revenue Assurance’ na kurekebisha she
ria ya TCRA kwa kuweka wazimakujumu ya TRA ndani ya TCRA, utaiingizia Serikali mapato ya takribani tshs660bn.
Mheshimiwa Spika
, katika eneo hili la Sekta ya Mawasiliano ninaomba kurejeakuitaka Wizara ya Fedha itoe maelezo hapa Bungeni namna ambavyo Hisa zaserikali katika Kampuni ya MIC Tanzania ltd inayomiliki Kampuni ya Tigo
zilivyouzwa. Mheshimiwa Spika Serikali ilikuwa inamiliki hisa asilimia 26 katikaKampuni hii. Kwa mujibu wa kumbukumbu nilizoziona Hisa hizi zote ziliuzwa kwathamani ya dola laki saba kwa mwana hisa mwenza mnamo mwezi Februarimwaka 2004. Kampuni hii leo inapata mapato ya Tshs bilioni 20 kwa mwezi,tuliuza hisa zetu asilimia 26 kwa dola laki saba! Laki Saba dola! Kambi yaUpinzani inataka uchunguzi maalumu katika mauzo haya na Taifa liambiwe ninikilitokea na hatua gani za kuchukua dhidi ya waliouza mali hii ya Umma bilazabuni wala kuzingatia thamani ya fedha.
Kuzuia mauzo ya ngozi ghafi nje ya nchiMheshimiwa Spika,
Kambi ya Upinzani imeshangazwa na hatua ya serikali kujana pendekezo la kuongeza ushuru kwenye bidhaa ya ngozi ghafiinayosafirishwa nje kutoka asilimia 40 hadi 90 lengo likiwa ni kuhamasishausindikaji wa ngozi hiyo na kuiongezea thamani.
Mheshimiwa Spika
, kwa nchi iliyo na mianya mingi ya rushwa kama Tanzaniahatua hii haitakuwa na tija kwa kuwa wafanyabiashara wengi wa ngozi ghafiwamekuwa na tabia ya kupunguza takwimu za kusafirisha ngozi ghafi na hivyokupelekea serikali kukosa mapato mengi sana. Serikali inafahamu kwamba hataushuru wa mauzo nje wa asilimia 40 haukuweza kutatua tatizo la viwanda vyandani kukosa malighafi. Kambi ya Upinzani haikubaliani na Pendekezo la Serikalikwani halitatatua tatizo la kukuza sekta ndogo ya Ngozi nchini.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani tunaitaka serikali kuzuia kabisa kusafirishangozi ghafi kwenda nje na badala yake kuwe na mpango wa kutumia ngozighafi hapa nchini na kuleta tija katika uchumi wa taifa kwa kutengeneza ajirana kuongeza thamani ya mauzo nje.
Mheshimiwa Spika
, hatua ya kuzuia ngozi ghafi kusafirishwa kwenda nje kwaTanzania itakuwa sio suala jipya kwa sababu Ethiopia imezuia na kuwekezakatika kiwanda cha viatu, mikanda na bidhaa za ngozi. Kutokana na Mpangowa Mendeleo ya Ethiopia (GTP
–
Growth and Transformation Plan) sekta yaNgozi itaingiza fedha za kigeni za thamani ya dola za Kimarekani bilioni 4 kwamwaka. Hii ni sawa na fedha za kigeni ambazo Tanzania inapata kutokakwenye Dhahabu na Utalii kwa pamoja. Ethiopia nchi iliyokuwa inatembea nabakuli na kulia njaa leo inakuwa nchi ya kupigiwa mfano na sisi Watanzania!Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda pia amepiga marufuku kuuza ngozighafi nje. Hata nchi ya Pakistani ambayo ndio ngozi zetu zinakwenda nayoimepiga marufuku mauzo ya ngozi ghafi nje. Serikali ipige marufuku Mauzo yangozi ghafi nje ya Nchi ili kulinda viwanda vya ngozi nchini, kuoongeza Ajira nakuongeza mapato ya Fedha za kigeni.
Kufuta Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa bidhaa za Maziwa
Mheshimiwa Spika, sekta ndogo ya Maziwa hapa nchini inahitaji kuwekewamaazingira ya kukua ili izalishe ajira na mapato ya kodi kwa Serikali. WakatiTanzania ndio nchi ya Afrika Mashariki inayoongoza kwa kuwa na
Ng’ombe
wengi lakini inaongoza kwa kuagiza maziwa kutoka nje yenye thamani ya dolaza kimarekani 3.6m. Wakati Kenya imelinda soko la Maziwa na Bidhaa zaMaziwa kwa kuondoa (zero rating) kodi ya VAT kwenye bidhaa za Maziwa,Waziri wa Fedha hajaonyesha kabisa juhudi zozote za kujengea uwezo sektandogo ya Maziwa hapa nchini na hivyo kuweza kuondolewa kabisa katikaushindani na kujikuta wafugaji wanakosa kabisa soko la kuuza maziwa yaohapa nchini. Nchi za Rwanda na Uganda pia zimelinda Maziwa na Bidhaa za

maziwa kwa njia hii. Ni muhimu Serikali kuwianisha kodi hii na Nchi nyingine zaAfrika Mashariki.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani inapendekeza kufanya marekebisho
kwenye sharia ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kufanya ‘
z
ero rating’
kwenye Maziwa na Bidhaa za Maziwa zinazozalishwa hapa nchini kwa kipindicha miaka 5 ili kufikisha uzalishaji wa angalau lita 500,000 za maziwa kwa sikukutoka lita 123,000 za sasa na kuweza kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfutatu.
Mheshimiwa Spika
, hatua zote za kuongeza mapato tulizopendekeza pamojana hatua za Bajeti Mbadala iliyopita ambazo tunarudia kuzipendekezazitaongeza Mapato ya Serikali kwa takribani shilingi bilioni 2,885 kamainavyoonyeshwa katika jedwali hapa chini.
NYONGEZA YA VYANZO VYA MAPATO MBADALA 2012/2013Chanzo cha Mapato Makisio - Bilioni
Marekebisho ya kodi za misitu ikiwemo Mkaa 130.8Kupunguza misamaha ya kodi, kuzuia ukwepaji kodi naudanganyifu wa Biashara ya Nje742.74Mauzo ya hisa za serikali 415.55Marekebisho ya kodi Sekta ya madini (kodi ya Mapato, Kodiya CGT na ushuru mbalimbali) (25% ya Mauzo ya Madini Nje)578.36Marekebisho ya Kodi na Usimamizi bora wa Mapato Kampuniza Simu502.26Marekebisho ya Kodi ya SDL 243.52Mapato ya wanyamapori 61.64
uondoa msamaha wa ushuru wa mafuta- kampuni zamadini44.9Usimamizi wa mapato ya utalii 51.75Kuimarisha biashara katika EAC kwa kuongeza mauzo 114.15
JUMLA 2,885.67Mheshimiwa Spika,
kama nilivyosema hapo juu, vyanzo hivi vya mapato nimjumuisho wa vyanzo ambavyo katika hotuba zetu mbadala za nyumatumekuwa tukipendekeza, ambapo tumevifanyia marekebisho kulingana nahali halisi ya uchumi ulivyo kwa sasa, pamoja na kupendekeza baadhi yamarekebisho ya sheria za kodi ili kuongeza mapato zaidi kwa Serikali.
DENI LA TAIFAMheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani inasikitika kwa serikali kuendeleakutengeneza madeni kwa Taifa kwa kuendelea kukopa zaidi kwa matumizi yakawaida ya serikali. Wakati Serikali inasisitiza kwamba Deni letu linastahmilika,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anaonyesha mashaka makubwa sanakutokana na kasi ya kukua kwa Deni la Taifa. Taarifa ya Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha kuwa Deni la Taifa linazidi kuongezekakwa asilimia 38 kutoka shilingi trillion 10.5 mwaka 2009/2010 hadi shilingi trillion14.4 mwaka 2010/2011. Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Deni la Taifa limefikiashilingi trillion 20.3 mpaka ilipofika mwezi Machi mwaka 2012. Ukisoma taarifa yaMwezi wa Mei 2012 ya Benki Kuu ya Tanzania, Deni la Taifa sasa limefikia shilingitrillion 22.
Mheshimiwa Spika
, Suala hapa sio ustahmilivu wa Deni kama inavyodai Serikalibali ni kwamba tunakopa kufanyia nini? Bajeti ya Mwaka 2012/13inayopendekezwa inaonyesha kwamba Serikali itakusanya shilingi trilioni 8.7kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi yakawaida. Ni dhahiri kwamba sehemu ya mikopo ambayo serikali inachukuasasa itakwenda kwenye matumizi ya kawaida. Hatutaki mikopo kwa ajili yamatumizi ya kawaida ya posho, kusafiri, magari nk. Tuchukue mikopo kuwekezakwenye miradi itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi. Bajeti inaonyeshakwamba Serikali itakopa shilingi takribani trillion 5 mwaka 2012/13. Serikali ikubalikutekeleza mapendekezo ya Kambi ya Upinzani ya kuimarisha ukusanyaji wakodi na kupanua wigo wa kodi katika maeneo muhimu kama sekta ya madinina mawasiliano, kuzuia misamaha ya kodi, kutokomeza ukwepaji kodi, nakuepuka matumizi mabaya ili kuepuka madeni yasiyo ya lazima.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani inapenda kusisitiza kwamba Bungelifanye ukaguzi maalumu kuhusu akaunti ya Deni la Taifa ili kuweza kubainiukweli kuhusu ustahmilivu wa Deni na mikopo ambayo Serikali inachukua kamainakwenda kwenye Maendeleo na miradi ipi na kama miradi hiyo ina tija.Vilevile tumependekeza kwamba Mikopo yote ambayo Serikali inachukua iweinapata idhini ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi au Bunge litunge shariaili kiwango cha juu cha kukopa ambacho Serikali haipaswi kuvuka. KuiachaSerikali inaendelea kukopa bila mpango ni kuliweka Taifa rehani na kupelekamzigo wa kulipa madeni haya kwa kizazi kijacho.
Hatuwezi kukubali Wazeewetu waishi maisha yao, waishi maisha yetu na pia wakope maisha ya watotowetu.
Mheshimiwa Spika
,Ukiangali sura ya Bajeti ya Serikali, inaonyesha kuwa Serikaliitakopa fedha zenye masharti ya kibiashara ndani na nje yenye thamani yaTshs. Trilioni 2.89 kwa kipindi hiki cha 2012/13. Athari ya mikopo ya kibiashara yandani ni kubwa sana kwa watanzania, kwanza inawafanya wananchi hasawajasiriamali wanaokopa kushindana na Serikali yao, kwani mabenkiyatashindwa kuwakopesha wafanyabiashara au wakikopa watakopa kwamasharti magumu na hasa riba kuwa kubwa. Jambo hili linapunguza uwezo wawazalishaji kuongeza uzalishaji hasa viwandani kwa kukosa mikopo yauendeshaji. Kama tulivyoshauri hapo juu, Serikali ijiepushe na mikopo yamasharti ya kibiashara kwa kuongeza makusanyo ya kodi.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani imepokea kwa masikitiko makubwataarifa ya Serikali kuwa imepata Mshauri Mwelekezi atakayeishauri katikakujiandaa kufanyiwa tathmini ya uwezo wa kukopa na kulipa madeni. Serikaliilieleze Bunge ni lini na kwa namna gani zabuni ya kumpata mshauri huyuilitangazwa na kama Sheria ya Manunuzi ilifuatwa.
Mwenendo wa Matumizi.
Mheshimiwa Spika, Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion)katika mwaka 2012/13 kama ilivyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi wikiiliyopita. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba mafungu ya juu 5yatakayoongoza kwa matumizi kwenye Bajeti hiyo ni Kama ifuatavyo;1. Huduma kwa Deni la Taifa Tshs 2.7 trilioni (USD 1.69 Billion)2. Wizara ya Ujenzi. Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)3. Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)Wizara ya Elimu Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)5. Wizara ya Nishati na Madini Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)
Jumla TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)
Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge
Mheshimiwa Spika
, Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajetiyote, kwa hiyo asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu na katiya hayo Wizara ni nne tu za Ujenzi, Elimu, Ulinzi na Nishati na Madini. Wizara yaKilimo wala Afya hazimo kabisa katika Wizara 5 zitakazopata fedha nyingi zaidikatika Bajeti. Fungu lenye kiwango kikubwa zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu22 ambalo ni malipo kwa Deni la Taifa. Pia sehemu kubwa ya fedhazilizotengwa kwa Ujenzi na Nishati ni madeni kwa wakandarasi wanaotekelezamiradi ya miaka ya nyuma. Shilingi bilioni 40 ambazo zimetengwa kwa ajili yaMradi wa Kiwira katika Wizara ya Nishati na Madini ni kwa ajili ya kulipia Madeniya Kampuni ya TanPower Resources ambayo iliuziwa Mgodi wa Kiwira nakushindwa kuundeleza.
Mheshimiwa Spika
, Madhara ya Deni la Taifa yanaonekana hapa katikamatuumizi ya Serikali ambapo tunapokuwa tunalipa madeni tunachukuwarasilimali fedha nyingi kutoka kwenye Miradi ya Maendeleo. Wakati Bajeti yaMaendeleo ni shilingi trilioni 4.5, Bajeti ya kugharamia Deni la Taifa ni shilingitrilioni 2.7 (sawa na nusu ya Bajeti nzima ya Maendeleo).
Mheshimiwa Spika
, Bajeti ya 2012/13 ni ya kulipa madeni zaidi kuliko Bajeti yakuchochea maendeleo ya Taifa letu. Bajeti hii pia yaweza pia kuwa ni Bajeti yakukopa zaidi maana jumla ya
TZS 5.1 trilioni (USD 3.19 Billion)
zitachukuliwa naSerikali kama mikopo kutoka vyanzo mbalimbali. Mikopo ya kibiashara ambayo
ni mikopo ghali sana itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedhauliopita.
Mheshimiwa Spika
, Mgawanyo wa rasilimali za nchi kwenye sekta zakipaumbele (Miundombinu ya usafirishaji kama reli, bandari, ndege viwanja vyandege n.k), Barabara, nishati,kilimo na mifugo, ili kuinua uchumi zimetengewafedha kidogo sana kuweza kuleta tija kulingana na malengo ya Mpango waMaendeleo kama ulivyopitishwa na Bunge lako tukufu. Bajeti iliyotengwa kwaajili ya nishati imeshuka kwa kiwango cha shilingi 40 bilioni, pia kwa mwakauliopita fedha zilizotengwa kwa ajili ya miundombinu,reli na TEHAMA zilitengwashilingi 2,781.4 bilioni kwa 2011/12 ikilinganishwa na shilingi 1,505.1 bilioni kwamwaka 2010/2011,(hili lilikuwa ni ongezeko la asilimia 85). Kwa bajeti ya mwakahuu inaonesha sekta zilezile za vipaumbele; bajeti iliyotengwa ni shilingi 1.394.5bilion ambayo ni pungufu ya asilimia 49.86 kwa kulinganisha na mwaka2011/2013.
Mheshimiwa Spika
, wakati Waziri wa Fedha analiambia Bunge kuwa ametengashilingi bilioni 1,383 kwa ajili ya Usafirishaji na Uchukuzi, Wizara ya Ujenziimetengewa shilingi bilioni 1,000 kati ya hizo. Wizara ya Uchukuzi yenye Reli,Bandari, Viwanja vya Ndege na Usafiri wa Maziwa ya Tanganyika, Nyasa naViktoria imetengewa chini ya shilingi bilioni 380. Serikali pia haijasema fedhaambazo zilitengwa na Bunge katika Bajeti inayomaliza muda wake nakuzielekeza kwenye Wizara ya Miundombinu na Wizara ya Uchukuzizimetumikaje maana bado wakandarasi wanadai na fedha za Reli hazikutokazote kama ilivyopitishwa na Bunge.
Mheshimiwa Spika
, wizara nyingi hazikupata fedha za Maendeleo kamazilivyopitishwa na Bunge. Halmashauri za Wilaya ndio zilipata hali mbaya zaidikatika kupata fedha za Maendeleo ambapo kwa wastani ni asilimia 47 tu ya
Bajeti ndio ilipelekwa katika Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa. Kutokanana hali hii Wabunge kama wawakilishi wa wananchi walihoji Serikali kwenyeKamati zao na kupata majibu ambayo sio ya kuridhisha hivyo kupelekeaWabunge kugomea baadhi ya Wizara.
Mheshimiwa Spika
, Ushahidi wa hayo ni baadhi ya Kamati za Kudumu zaBunge kukataa kukubali Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa baadhi yaWizara zilizo chini ya Kamati hizo. Wizara ambazo hazikupitishiwa /Kukubaliwamakadirio yake ni pamoja na;
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Wizara ya Uchukuzi, na (nilishangaa kumwona Waziri wa Uchukuziakiwaahidi wananchi pale Jangwani kwamba Reli inakarabatiwa vyakutosha ilhali Kamati haijapitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara yakekwa kuwa haikupewa fedha za kutosha)
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
Mheshimiwa Spika
, kabla Bunge lako tukufu halijajadili Makadirio ya Matumizi yamwaka unaokuja ni vema Serikali itueleze kwanza fedha zilizotengwa mwakauliopita na hazikufika hatima yake nini?
Mheshimiwa Spika,
uwiano wa bajeti iliyotengwa kwa matumizi ya kawaidaambayo ni asilimia 70% wakati bajeti ya maendeleo asilimia 30% haiwezeshinchi kupiga hatua ya haraka ya Maendeleo. Kama ilivyoonyeshwa na WaziriKivuli Mipango na nitakavyohitimisha hotuba hii, Serikali imetayarisha Bajeti hiibila kuzingatia masharti yaliyowekwa na Mpango wa Maendeleo uliopitishwana Bunge kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu ibara ya 63 (3)(c) kwa kutotengaasilimia 35 ya Mapato ya ndani ya Serikali kwenye Bajeti ya Maendeleo.
Mheshimiwa Spika
, Serikali imekuwa ikitenga fedha kidogo katika miradi yamaendeleo katika bajeti zake. Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), matumizi ya kawaida ya Serikaliyanaongezeka huku matumizi katika shughuli za maendeleo yanapunguamwaka hadi mwaka. Takwimu katika jedwali hapa chini zinaonyesha
Fungu 2009/2010 % 2010/2011 %
Fedha za matumiziya kawaida (Sh) 6,251,629,581,428 73 7,587,424,923,903 77Fedha za matumiziya maendeleo (Sh) 2,299,010,652,135 27 2,223,684,150,465 23
Jumla 8,550,640,233,563 100 9,811,109,074,368 100
Chanzo: Ripoti ya CAG, uk. 21Aidha, kwa miaka miwili iliyopita yaani 2009/2010 na 2010/2011 kumekuwahakuna uwiano wa fedha za Maendeleo kama bajeti zilivyopitishwa na Bungedhidi ya fedha zinazotolewa na hazina kwa ajili ya maendeleo katika Wizara naIdara. Tazama jedwali;Mwaka Bajeti iliyoidhinishwa Fedha halisizilizotolewaTofauti (Sh) %2009/2010 2,825,431,400,000 2,299,010,652,135 526,420,747,865 192010/2011 3,750,684,569,000 2,223,684,150,465 1,527,000,418,535 41Chanzo: Ripoti ya CAG, uk.22
Mheshimiwa Spika
, Kutokana na takwimu hizi, jumla ya Sh. 1,527,000,418,535 auasilimia 41 ya fedha zilizoidhinishwa kwa maendeleo hazikutolewa katika
mwaka wa fedha 2010/2011, na kiasi cha Sh. 526,420,747,865 au asilimia 19 yafedha zilizoidhinishwa mwaka 2009/2010 hazikutolewa pia. Hii ina maana kuwashughuli za maendeleo za kiasi hicho cha fedha hazikutekelezwa kwa miakahusika.
Mheshimiwa Spika,
Kambi ya Upinzani inatafsiri hali hiyo kama utovu mkubwawa nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa upande wa Serikali, Vilivileinaonesha ni jinsi gani Serikali yetu haithamini maendeleo ndio maana kilamwaka Serikali inazidisha matumizi yake na kuhakikisha kuwa inayapata kwawakati huku ikipunguza bajeti ya maendeleo na kutotoa fedha zote kamazilivyoidhinishwa na mbaya zaidi hata zile zinazotolewa hazitolewi kwa wakatimuafaka. Hii inafanya kukaa hapa Dodoma na kupitisha Bajeti kuwe hakunamaana maana Bajeti haitekelezwi kama ilivyopitishwa.
Mheshimiwa Spika
, Kiasi kinachotengwa kwa ajili ya maendeleo kimeshukakutoka shilingi trilioni 4.9 katika mwaka wa fedha 2011/12 hadi kufikia kiasi chashilingi trililioni 4.5 mwaka huu wa fedha 2012/13. Pamoja na serikali kushindwakutekeleza miradi ya maendeleo katika bajeti iliyopita, bado imeendeleakupunguza bajeti ya maendeleo katika bajeti hii. Ni dhahiri serikali haizingatiiswala la maendeleo ya mwananchi, pia kutoona njia ya kuweka mkazo katikamaendeleo na kuendelea kupuuzia maazimio ya mpango wa maendeleo wamiaka mitano.
Mheshimiwa Spika
, katika Bajeti mbadala, Kambi ya Upinzani imetenga asilimia36.06 na kukidhi matakwa ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kutoka katikamapato ya ndani kwa matumizi ya maendeleo kama Mpango wa Maendeleoya Taifa ulivyoelekeza.
Mheshimiwa Spika
, Tuliamua kama Taifa kwamba Mpango wa Maendeleo wamiaka mitano ndio safina yetu ya kuelekea nchi ya ahadi (middle incomecountry). Mpango ukapitishwa na Bunge na kuwekwa sahihi na Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania. Inasikitisha kuona kuwa Serikali inatoboa kisiri sirisafina hii wakati tupo kati kati ya maji! Ninaamini wananchi wanawaonawanaotoboa safina yetu na watawatosa kabla hawajazamisha Taifa zima kwakushindwa kutekeleza Mpango unavyoelekeza.
Ubadhirifu wa fedha zinazotengwa
Mheshimiwa Spika
, pamoja na fedha za maendeleo kutolewa kidogokulinganisha na bajeti inayopitishwa na Bunge, bado kumekuwepo na matumiziyasiyo na tija na ubadhirifu mkubwa.
Mheshimiwa Spika
, upotevu wa fedha za umma umeendelea kuwa kikwazokikubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi. Uchambuziwetu juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)kwa mwaka 2010/2011 pekee, umebaini takribani jumla ya Bilioni 12.9(12,968,168,985) za fedha za umma zimepotea kama ongezeko kutoka shilingibillion 11.9 (11,152,048,065) ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 14 yaupotevu wa fedha za Serikali kwa mwaka wa fedha 2009/2010,hii inaonyeshakuwa Serikali inaona ni jambo la kawaida kupoteza viwango hivi vya pesa zaSerikali na kambi ya upinzani kuwasisistiza wananchi kuendelea kuitathminiSerikali yao sasa ili kuweza kufanya maamuzi sahihi dhidi ya Serikali yao.
MAPENDEKEZO YA KAMBI YA UPINZANISERA YA MATUMIZI 2012/13 KWA BAJETI MBADALAMheshimiwa Spika
, lengo kuu la Bajeti Mbadala ni kuhakikisha uchumi unakuakatika maeneo ya vijijini kwa kati ya asilimia 6 na 8 ili kuleta Maendeleo yawananchi na kutokomeza umasikini. Kwa njia hiyo ni dhahiri wananchiwapatao milioni 30 waishio vijijini watanufaika na matumizi ya raslimali zao.
Vipaumbele vya bajeti ya Matumizi.
(i)
Kujenga Mazingira ya Ukuaji wa uchumi vijijini (rural growth) kwakuboresha miundombinu ya umeme, barabara, maji namiundombinu ya Umwagiliaji. Tunapendekeza kutumia shilingi bilioni600 kila mwaka (bilioni 150 kwa kila sekta niliyotaja). Fedha hizizitasimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo Vijijini (RuralDevelopment Authority
–
to be established) itakayokuwa chini yaOfisi ya Waziri Mkuu.(ii)
Kukarabati Reli ya Kati na matawi yake ya Tanga/Arusha naMpanda. Tutatenga tshs 443bn kwa RAHCO kwa ajili ya Reli. Lengoni kuhakikisha Reli ya Kati inafikia uwezo wa kusafirisha Tani 1.5mkwa mwaka na hivyo kulipatia Taifa fedha za kigeni katika sekta yausafirishaji kupitia Bandari ya Dar es Salaam. Tunataka sekta yausafirishaji iliingizie Taifa fedha za kigeni mpaka dola za kimarekani1.5 bilioni kutoka dola 0.5 bilioni za sasa.(iii)
Kuboresha Elimu na Afya hasa kwa Shule na Zahanati/Vituo vyaAfya vya Vijijini kwa kutoa motisha kwa wafanyakazi wa Sekta hiziwalio kwenye Halmashauri za Wilaya. Tunapendekeza posho za
Mazingira ya Vijijini kwa Walimu, Madaktari na Manesi sawa namara moja na nusu ya Mishahara yao. Vile vile tutaongezamishahara ya Walimu, Manesi na Madaktari kwa asilimia 50,pamoja na kuboresha stahili zingine za kazi ili kuvutia Watanzaniawengi zaidi katika maeneo haya na kuboresha huduma zao kwawananchi.(iv)
Kuongeza Kima cha chini cha Mshahara kwa Wafanyakazi waUmma mpaka Tshs 315,000 kwa Mwezi(v)
Kuanzisha Pensheni ya uzeeni kwa Wazee wote nchini wenye umriwa zaidi ya miaka 60.(vi)
Kujenga Uwezo wa Viwanda vya ndani ili Kuuza nje bidhaa zakilimo na mifugo zilizoongezewa thamani. Tutazuia kuuza njeKorosho ghafi na Ngozi ghafi kwa kuanzia. Lengo ni kufufuaviwanda vyote vya nguo na kuanzisha viwanda vipya kwa kutoamotisha kwa wawekezaji watakaotumia malighafi za hapa nchini.(vii)
Kupunguza mzigo wa matumizi ya magari ya Serikali kwa kupiga
mnada baadhi ya ‘mashangingi’ na kuweka mfumo wa
kukopeshaMagari kwa watumishi wote wa Umma wanaostahili Magari kamaalivyofanya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania. Katika Taarifa yakekwa Kamati ya Fedha na Uchumi, Waziri wa Fedha alitamka,
‘….kufanya mapitio ya stahili za aina za magari kwa viongozi wa
ngazi mbalimbali na kuandaa mwongozo wa kugharamia ununuziwa vyombo vya usafiri ili kupunguza matumizi ya magari, mafuta na
matengenezo ya magari…’ kama hatua za kubana matumizi.
Hatua hii ya kupunguza gharama za magari Waziri hakuisemakabisa katika hotuba yake Bungeni.
Kuendelea kusisitiza kufutwa kwa posho za vikao katika mfumomzima wa malipo na stahili kwa watumishi wa Umma. Katika Taarifa
yake kwa Kamati ya Fedha, Waziri wa Fedha alitamka ‘…. Kufanya
mapitio ya posho na stahili zote kwa lengo l
a kuziwianisha….’
Sualahili nalo Waziri hakulizungumza kabisa katika Hotuba yake Bungeni.(ix)
Kuanzisha Chuo Kikuu cha Mtwara (Mtwara University for PetroleumStudies) ili kuzalisha wataalamu wa kutosha wa Sekta ya Mafuta naGesi na kuliandaa Taifa kuwa na wasomi mahiri wa maeneo hayona hivyo kufaidika na Utajiri wa Mafuta na Gesi uliopo nchini kwetu.Tunapendekeza shilingi bilioni 200 mwaka huu katika Bajeti yaWizara ya Elimu kwa ajiri ya Mradi huu.(x)
Kutunga sheria mpya ya Mashirika ya Umma (Public CorporationsAct) ili kujengea uwezo Ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamiavyema Mashirika yote ya Umma ambayo Serikali inamiliki kwa zaidiya asilimia 100 na kutoa nguvu za kisheria kwa Shirika la CHCkuweza kusimamia hisa za Serikali katika Kampuni na Mashirikaambayo Serikali inamiliki chini ya asilimia 50.(xi)
Kupunguza gharama za safari za nje kwa kupunguza ukubwa wamisafara na madaraja ya kusafiria. Eneo hili la safari za njelimekuwa likiigharimu Serikali fedha nyingi sana.
Mheshimiwa Spika
, kufuatia hatua mbali mbali za kikodi tulizozichukua Kambi yaUpinzani inapendekeza Bajeti ya shilingi trilioni 15 ambazo zitapatikana kwaMapato ya ndani ya shilingi trilioni 11.9 na misaada na mikopo ya kibajeti yashilingi trilioni 3.2 kama ilivyopendekezwa na Serikali. Kambi ya Upinzaniinapendekeza Serikali kutokukopa kibiashara ili kudhibiti ukuaji wa Deni la Taifa
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba Serikaliitatumia shilingi trilioni 9 katika Matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 6 kamaMatumizi ya Maendeleo. Katika fedha za Maendeleo, asilimia 35 ya Mapato yandani yameelekezwa huko kama ilivyoagizwa na Mpango wa Maendeleo yaTaifa ulioidhinishwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba.
SURA YA BAJETI MBADALA YA MWAKA 2012/2013MAPATO SHILINGI MILIONIA Mapato ya ndani 11,889,078
i)mapato ya kodi (TRA)ii)Mapato yasiyo ya kodi
B
Mapato ya Halmashauri
C
Mikopo na Misaada ya kibajeti (GBS) 842,487
D
Misaada na mikopo ya miradi ya maendeleonay a kisekta2,314,231i)Misaada 1,465,461ii)Misaada na mikopo kisekta 415,137iii)MCC(MCA-T) 433,634
Jumla ya Misaada na mikopo ya kibajeti 3,156,718JUMLA YA MAPATO YOTE. 15,045,796MATUMIZIE Matumizi ya Kawaida 9,000,000H Matumizi ya Maendeleo
(i)Fedha za ndani 4,161,177
‘
Licha ya kwamba tunahitaji ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi. Changamoto sasa ni namna ganiukuaji huu wa uchumi unawafikia wananchi milioni thelathini wa Vijijini na kuboresha maisha
yao.’
Zitto Kabwe, Waziri Kivuli wa Fedha, Tanzania.
35
(ii)Fedha za Nje 1,884,619
Jumla ya matumizi ya maendeleo 6,045,796JUMLA YA MATUMIZI YOTE. 15,045,796HitimishoFedha za RadaMheshimiwa Spika,
Wakati Kamati za Bunge zilipokaa kujadili taarifa ya Serikalikuhusu Mfumo wa Mapato na Matumizi, Waziri wa Fedha na Uchumi alitoaTaarifa kuhusu Fedha za Rada zilizorejeshwa, jumla ya shilingi 72.3 bilioni ambazozilipokelewa tarehe 26 Machi, 2012. Kwa mshtuko wa Wabunge, Waziri aliiambiaKamati kuwa mchakato wa manunuzi ya vitabu na madawati kwa kutumiafedha hizi ulikuwa umeanza chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI. Fedha hizihazijawahi kupitishwa na Bunge lako tukufu. Kitendo cha Serikali kuzitumia kablaya kupitishwa na Bunge ni kuvunja sheria za Fedha kuhusiana na masuala yaBajeti. Wakati Waziri akiwasilisha Hotuba yake hakugusia kabisa suala la fedhazilizorejeshwa kutokana na Ununuzi wa Rada!
Mheshimiwa Spika,
Kambi ya upinzani inataka maelezo ya Serikali juu ya Fedhahizi na utaratibu wa kuzitumia. Kambi inataka kufahamu vigezo vilivyotumikakuteua mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam kutumia fedha hizi.Kambi pia inapenda kufahamu Deni lililochukuliwa kununua Rada hii iliyoletakashfa kubwa sana hapa nchini limefikia kiasi gani kulilipa na tukililipa tutakuwatumelipa kiasi gani kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika,
Uumbaji wa bajeti ya Serikali umekuwa ni ule ambaounapendelewa zaidi na wale wavivu wa kufikiri, yaani mfumo rahisi, wataalamuwanauita
Incremental Budgeting
.
Mfumo huu hujikita zaidi katika kutizamaukuaji wa mapato na kugawa mapato hayo kwa mtindo wa nyongeza yaasilimia Fulani toka katika bajeti iliyotangulia. Mfumo huu huacha kuzingatiamambo mengi mtambuka. Mfano, tunaweza tizama sekta mojawapo yaumeme ambapo tukifanya uumbaji wa bajeti kwa mfumo wa kiasi chanyongeza (incremental budget) kuna thamani halisi ambazo ukizitizama kwabei wazi ya soko tayari zimepaa sana ndani ya miezi kumi na miwili.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani Bungeni, tukiwa ni serikali ambayotunasubiri kukabidhiwa dola, tunapendekeza kwamba ni vema tukaanzakutizama uwezekano wa matumizi ya
Zero Budgeting
ambapo japo ni mfumoambao unahitaji kazi ya ziada, lakini una faida sana kwani hutizama mipangoya matumizi kulingana na wakati uliopo huku ikifanya rejea ya wakati uliopita.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya Upinzani pia inapendekeza kwamba Bajeti zaMashirika ya Umma ziwe sehemu ya Bajeti Kuu ya Nchi kwani kuna masualamengi yanayotekelezwa na Mashirika haya na Wananchi kupitia Bungehawayajui. Ni vema katika mfumo mpya wa Bajeti tutakaokuwa nao kufuatiamapendekezo ya Spika wa Bunge ambapo kutakuwa na Ofisi ya Bajeti yaBunge na Kamati ya Bunge ya Bajeti, Sheria ya Bajeti (Fiscal ResponsibilityAct/Budget Act) izingatie suala la kuziweka kama viambatisho Bajeti zaMashirika ya Umma katika Bajeti ya Nchi.
Mheshimiwa Spika
, Bajeti ya Serikali ya mwaka huu kama ilivyowasilishwa naWaziri wa Fedha imewasahau kabisa wananchi wa vijijini na haina mkakatiwowote wa kuwakomboa watanzania walio wengi wanaoishi huko. Mipango
mingi ya kikodi katika sera ya Mapato ya Serikali itasaidia wakazi wa mijiniambao ni asilimia 25 tu ya Watanzania wote.
Mheshimiwa Spika
, Kambi ya upinzani inapenda kuweka msisitizo kwambaTanzania bado ni nchi ya Wakulima maana robo tatu ya Watanzania wanaishivijijini ambapo hawajui hizi hadithi za Uchumi kukua tunazoimba na kupewa sifakila siku. Hawa ni watu milioni 30 ambao hawana Maji, hawana Umeme, mazaoyao hayafiki sokoni maana hawana barabara nzuri, shule wanazosoma watotowao hazina walimu maana wanakimbia mazingira magumu. Hawa Watanzaniawa chini milioni 30 (The Bottom 30M) tunaowawakilisha hawana bima mazaoyakiharibiwa na wala hawana pensheni wanapokuwa wamezeeka na
kupoteza nguvu za kufanya kazi. Hawa ‘The Bottom 30M’ bado wanaishi maisha
walioshi babu zetu. Hawa Watanzania milioni 30 tumewasahau. TunajengaMataifa mawili ndani ya nchi moja, moja la mafukara (wanavijiji) na moja lawanaojiweza (wamijini).
Mheshimiwa Spika
, Kama tunataka kujibu kitendawili cha kuwa na Uchumiunaokua kwa kasi lakini haupunguzi umasikini inabidi kuelekeza nguvu zetu vijijiniwalipo Watanzania wengi. Kukuza Uchumi wa Vijijini kwa kuwekeza kwenyemisingi ya kujenga uchumi imara ndio njia pekee ya kutokomeza ufukara waWatanzania.
Mheshimiwa Spika
, Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani mwaka huu ni Bajetiya Ukombozi wa mwananchi. Licha ya kwamba tunahitaji ukuaji wa kasi zaidiwa uchumi. Changamoto sasa ni namna gani ukuaji huu wa uchumi unawafikiawananchi milioni thelathini wa Vijijini na kuboresha maisha yao.
Mheshimiwa Spika,
KWA KUWA Mpango wa Maendeleo wa miaka mitanouliwasilishwa Bungeni na Serikali na kupata pongezi nyingi sana kutoka kwa

waheshimiwa wabunge lakini cha kushangaza Serikali hii ya Chama ChaMapinduzi imeshindwa kuutekeleza kwa vitendo mpango huu wa Taifa. Mwakawa kwanza Mpango haukuwekewa fedha kwa kuwa ulikuwa wa Mpito.Mpango unahitaji angalau shilingi trillion Nane kila mwaka ili uwezekutekelezwa. Mpango ulipata shilingi trillion moja tu mwaka 2011/12.
Mheshimiwa Spika
, KWA KUWA Bunge liliazimia namna ya kuhakikisha tunapatafedha za kuendeleza nchi yetu sisi wenyewe, naomba kunukuu ukurasa wa 92kifungu cha 4.3.1 katika Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano toleo lakiswahili kama ifuatavyo
‘kwa kuelewa kuwa wakati wote kutakuwa na miradi
ya uwekezaji nje ya mpango, serikali, kuanzia sasa, itakuwa inatenga
asilimia 35ya makadirio ya mapato yake ya ndani
kwa ajili ya kugharamia bajeti ya
maendeleo kila mwaka’
mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika,
KWA KUWA katika makadirio ya Bajeti ya Serikali kwamwaka wa Fedha 2012/13
Serikali imetenga asilimia sifuri ya Mapato ya ndanikwa ajili ya kugharamia Bajeti ya Maendeleo
. Serikali hii imeshindwa kusimamiaahadi zake yenyewe kama inavyoonekana katika mpango wa maendeleo yamiaka mitano. Serikali hii ya CCM imeshindwa kuheshimu Uamuzi uliopitishwa naBunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka1977.
Mheshimiwa Spika
, KWA KUWA Kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(c ) madaraka yaBunge ni pamoja na
‘
Kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefuau wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano,
na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo”.
Bungeliliidhinisha Mpango kwa mujibu wa ibara tajwa ya Katiba
Mheshimiwa Spika
, KWA KUWA Bajeti ya mwaka 2012/13 iliyowasilishwa Bungenina Waziri wa Fedha na Uchumi haikukidhi matakwa ya Mpango wa Maendeleokama ambavyo ulipitishwa na Bunge, HIVYO BASI,Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali iiondoe (withdraw) Bungeni Bajetiiliyoileta ili ikatayarishwe upya ili ikidhi matakwa (compliance) ya Mpango waMaendeleo kama ulivyoidhinishwa na Bunge na kusainiwa na Rais wa nchi.
Mheshimiwa Spika Naomba Kuwasilisha
………………………………………………….
Kabwe Zuberi Zitto, MbWaziri wa Fedha na Uchumi Kivuli18.06.2012
SURA YA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2012/2013.MAPATO % SHILINGI MILIONIA Mapato ya ndani 57.63 8,714,671
i)mapato ya kodi (TRA) 8,070,088ii)Mapato yasiyo ya kodi 644,583
B Mapato ya Halmashauri 362,206C
Mikopo na Misaada ya kibajeti (GBS)
5.57
842,487
D
Mikopo na misaada ya miradi ya maendeleo na yakisekta
15.30
2,314,231
E
Mikopo ya ndani
10.78
1,631,231
F
Mikopo yenye masharti ya kibiashara
8.25
1,254,092
JUMLA YA MAPATO YOTE. 15,119,644MATUMIZIE Matumizi ya Kawaida 71.06 10,591,805(i)
Deni la taifa 2,745,056(ii)
Mishahara 3,781,100(iii)
Matumizi Mengineyo 4,065,649
Wizara 3,311,399Mikoa 49,701Halmashauri 704,549
H Matumizi ya Maendeleo
(i)Fedha za ndani 2,231,608(ii)Fedha za Nje 2,34,231
Jumla ya matumizi ya maendeleo 29.94 4,527,839JUMLA YA MATUMIZI YOTE. 15,119,644
TOFAUTI KATI YA BAJETI YA SERIKALI NA BAJETI MBADALA YA KAMBI RASMI YA UPINZANIBajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani2012/2013 Bajeti ya Serikali kwa mwaka wafedha 2012/2013
Kukuza uchumi vijijini. Mwelekeo na malengo ya Serikalihauleweki, hatua zilizochukuliwa nikoboresha uchumi wa mijini.Njia mbadala zinazotekelezeka za kupunguzamfumuko wa bei.Kuwa na njia zilezile zilizoshindwamwaka wa fedha uliopita zakupunguza mfumuko wa bei.Kunufaika
na mapato ya mitaji “Capital gains”
Kutoza hisa kwa mauziano ya hisa
‘
Licha ya kwamba tunahitaji ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi. Changamoto sasa ni namna ganiukuaji huu wa uchumi unawafikia wananchi milioni thelathini wa Vijijini na kuboresha maisha
yao.’
Zitto Kabwe, Waziri Kivuli wa Fedha, Tanzania.
41
kwa kutoza kodi kwa mali za kampuni zilizoponchini kwa mauzo yanayofanyika nje ya nchina hivyo kupanua wigo wa TRA kutoza kodipekee kwa mauziano yanayofanyikanje. Hisa inapunguza wigo wa TRAkutoza kodi.Kupanua wigo wa kodi ya tozo la ujuzi(SDL)kwa kuijumuisha serikali na mashirika yaumma na kupunguza mzigo kwa sekta binafsipekee.Kupitia upya SDL bila kuonyeshanamna itakavyofanyika.Kupunguza misamaha ya kodi kutoka 3% yasasa hadi 1% ya pato la taifa.Kurudia ahadi zilezile za mwaka janaza kupitia upya misamaha ya kodibila kuleta mrejesho wa kilewalichokifanya.Kuboresha kodi sekta ya madini ili kupelekeataifa kupata nagalau 25% ya mazuo ya madininje kama mapato ya serikali.Kutokuwa na hatua yoyote yakuongeza mapato ya Serikali kutokakatika sekta ya madini.Kulipa kima cha chini cha mshahara kuanziashilingi 315,000.Kulipa shilingi 170,000 kama kima chachini.Kulipa pensheni kwa wazee wote kuanziamiaka 60 na kuendeleaKutokuwa na mfumo wa penshenikwa wote.Kushusha kiwango cha chini kodi ya mapatokwa wafanyakazi (PAYE) kutoka 14% hadi 9% ilikumpunguzia mfanyakazi makali ya maisha nakutoza kodi zaidi kwa watu wenye kipatokikubwaKubaki na kiwango kilekile cha chinicha kodi ya 14% na kubakiza mfumoule ule wa kodi ya Mapatounaomfanya Masikini alipe zaidi yaTajiri.Kuziba mianya kwa makampuni ya simukukwepa kutokulipa kodi ya mapato.Kuongeza ushuru wa bidhaa kwenyemuda wa maongezi na hivyokumwongezea gharamamwananchi.Kuondoa mikopo ya kibiashara ili kulipunguzia Kuendelea mikopo na hivyo
‘
Licha ya kwamba tunahitaji ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi. Changamoto sasa ni namna ganiukuaji huu wa uchumi unawafikia wananchi milioni thelathini wa Vijijini na kuboresha maisha
yao.’
Zitto Kabwe, Waziri Kivuli wa Fedha, Tanzania.
42
taifa mzigo wa madeni kuongeza deni la taifa. mingi yakibiashara.Kutenga asilimia 35 ya mapato ya ndani kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleokama ilivyoelekezwa kwenye mpango wamaendeleo wa miaka mitano.Kutenga asilimia sifuri ya fedha zamapato ya ndani kwa ajili ya miradiya maendeleo na hvyokutokutekeleza mpango wa taifa .Utegemezi wa Bajeti 21.3% Utegemezi wa Bajeti 42.37%
JEDWALI LA ULINGANISHO WA ASILIMIA KWA BAJTEI MBILIUPINZANI ASILIMIA SERIKALI ASILIMIAA.
Mapato ya ndani
78.70 Mapato ya ndani
57.63B.
Mikopo na Misaada yakibajeti (GBS)
5.57
Mikopo na Misaada yakibajeti (GBS)
5.57C.
Misaada na mikopo ya miradiya maendeleo na y akisekta
15.30
Misaada na mikopo yamiradi ya maendeleo na y aKisekta
15.30D.
Mikopo ya masharti yakibiashara ya ndani
0
Mikopo ya masharti yakibiashara ya ndani
10.78E.
Mikopo ya masharti yakibiashara ya nje.
0
Mikopo ya masharti yakibiashara ya nje.
8.25F.
Matumizi ya Kawaida
59.22 Matumizi ya Kawaida
71.06
‘
Licha ya kwamba tunahitaji ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi. Changamoto sasa ni namna ganiukuaji huu wa uchumi unawafikia wananchi milioni thelathini wa Vijijini na kuboresha maisha
yao.’
Zitto Kabwe, Waziri Kivuli wa Fedha, Tanzania.
43
G
Matumizi ya Maendeleo
40.78 Matumizi ya Maendeleo
29.94H.
Matumizi ya maendeleofedha za mapato ya ndani
36.06
Matumizi ya maendeleofedha za ndani
0I.
Matumizi ya maendeleofedha za nje
12.39
Matumizi ya maendeleofedha za nje
29.94
Subscribe to:
Posts (Atom)