Tuesday, June 19, 2012


Zitto Kabwe.
Kambi rasmi ya upinzani bungeni imewasilisha bajeti mbadala ya kambi hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na kuitaka serikali kuwa makini katika kukopa nje ya nchi kutokana na kukua kwa kasi kwa deni la taifa na kupendekeza pia magari ya kifahari ya serikali yapigwe mnada ili kupunguza matumizi ya mafuta.
Pamoja na hizo ishu kambi hiyo imeitaka serikali kuainisha njia za kudhibiti mfumuko wa bei unaowaongezea mzigo wananchi na kuwaongezea mishahara walimu, madaktari na wauguzi kwa asilimia 50 huku ikiweka mpango wa kuanza kuwalipa pensheni wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa ruhusa ya Chadema Zitto Kabwe ambae pia ni waziri kivuli wa fedha amesema “swala ni kwamba tunakopa ili kufanya nini? bajeti ya mwaka 2012/2013 inayopendekezwa inaonyesha kwamba serikali itakusanya trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida, ni dhahiri kwamba sehemu ya mikopo ambayo serikali inachukua sasa itakwenda kwenye matumizi ya kawaida, hatutaki mikopo kwa ajili ya matumizi ya posho”
Kabwe amekamilisha kauli yake akikaririwa akisema “tuchukue mikopo kuwekeza kwenye miradi itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi, kuiacha serikali kuendelea kukopa bila mpango ni kuliweka taifa rehani, hatuwezi kukubali wazee wetu waishi maisha yao waishi maisha yetu na wakope maisha ya watoto wetu”
Wabunge mbalimbali walichangia bungeni Dodoma June 18 2012 na kulalamikia kuongezeka kwa deni la taifa, usimamizi mbaya wa rasilimali za nchi na ugumu wa maisha kwa mtanzania na wengine wakakataa kuiunga mkono bajeti hiyo.


.
Ikiwa ni wiki moja tu imepita toka kutokea ajali ya Helikopta huko Kenya iliyochukua maisha ya watu sita wakiwemo mawaziri wawili, asubuhi ya June 18 2012 wasiwasi ulienea tena  kwenye mji wa Karatina huko Kenya baada ya HELIKOPTA kutua ghafla shambani kutokana na hali mbaya ya hewa kwenye anga.
Standard Media wamesema mwandishi wao wa eneo la mlima Kenya amesema hiyo helikopta ni ya raia wa kigeni aitwae Allan Root  aliekua akiwapeleka watoto wake shule Nairobi.
Root anaishi kwenye eneo la Mbuga ya LEWA na alipofika eneo la Karatina alilazimika kutua kwa ghafla katika shamba moja eneo la Mathaithi karibu na Karatina kutokana na hiyo hali mbaya ya anga ambayo kama angeendelea kusafiri kulikua na uwezekano mkubwa wa ajali kutokea.


Laurent Blanc.
Stori kwenye kila mtaa unaofatilia soka la nje hazikosi jina la club ya Tottenham ambayo imempiga chini juzi kocha wake ambae ni Harry Redknapp na sasa inatafuta kichwa kipya kwa ajili ya hiyo nafasi.
Sky Sports wamesema club hiyo sasa hivi imeweka macho yake kwa kocha wa Ufaransa Laurent Blanc (46) ambae mkataba wake na Ufaransa unakwisha baada ya michuano ya Euro ambapo inaaminika anaweza kurudi kwenye Premier League.
Kwa sasa wako kwenye mazungumzona Laurent japo sio kocha peke yake ambae wanafanya nae mazungumzo, kuna kocha wa zamani wa Chelsea Andre Villa Boas na kocha wa Everton David Moyes… acha tusubiri tuone matokeo.


Bmw M6 2012
.
.
.
.
.
.


 
.
Serikali imetolea ufafanuzi ishu ya mkwanja ambao ni shilingi bilioni 3.5 ulioidhinishwa na wizara ya mambo ya nje yna ushirikiano wa kimataifa pamoja na utumishi wa umma kwa ajili ya safari ya Rais Jakaya Kikwete kuelekea nje ya nchi, pesa ambazo zilidaiwa kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha  March mwaka huu.
Waziri wa wizara hiyo Bernard Membe baada ya kukutana na washika kalamu amesema fedha zote zimerejeshwa wizarani na kwamba tayari wizara imeunda kamati kuchunguza utaratibu uliotumika kuidhinisha fedha hizo, na kuongeza kwamba wakati wa uidhinishwa wa hizo fedha viongozi wote wa ngazi za juu wa wizara pamoja na muhasibu mkuu hawakuwepo.
Amesema “hizi fedha zote ziliingia kwenye account ya wizara na nyingine zikaletwa wizarani lakini hata senti moja haikuchukuliwa, tuliziona na zikahesabiwa na zilizofika hapa wizarani kwa nia ya safari zilirejeshwa benki kwa hiyo hayupo alieiba, tusimuhukumu mtu ambae hajaiba bado”
Kuhusu ishu yake kwamba amekitabiria chama cha CHADEMA ushindi katika uchaguzi mkuu ujao, Membe amesema  “ni kitu ambacho kiliwekwa makusudi ili kunifitinisha na Chadema na Wanaccm wenzangu nionekana wa ovyo tu nisikaribishe karibishe watu, hamna nitaendelea kukaribisha watu nyumbani kwangu… vijana wa Chadema walikuja kwa heshima zote nyumbani kwangu bahati nzuri walikuja wakati wa mlo wa mchana kama waliotea nikawakaribisha nilikua na marafiki zangu, walifurahi vizuri kweli”


.
Msichana wa miaka 16 nchini Kenya amefanya kituko baada ya kukosea na kupika bangi kama mboga kwa ajili ya chakula cha familia jioni huko Kiarimui kwenye wilaya ya Embu..
Standard Media wamesema baba mzazi wa huyo binti ambae ni mwalimu wa sekondari ana shamba nyumbani ambalo lina mboga mbalimbali ambazo huwa zinanawiri wakati wote, kiangazi na vuli.
Jioni hiyo mama wa huyo binti alimuagiza mwanae ambae amerudi nyumbani kwa likizo kwenye kupika ugali na mboga za majani, sasa mtoto alipokwenda shambani kuchukua mboga hakuweza kutofautisha bangi na mchicha.
.
Sasa noma ikawa kwenye msosi baada ya kuiva ambapo mtoto wa mwisho wa hiyo familia ambae ni wa kiume alianza kucheka kucheka ovyo na ndio alikua wa kwanza wa kupakua msosi mezani, alipomaliza kupeleka matonge mawili akasikia usingizi na kuzimika hapohapo, wengine pia walipakua msosi na kweli na wao wakaanza kucheka cheka ovyo.
Kingine cha ajabu wakati wako mezani kuna mjusi alipita ukutani alafu wote wakaanza kucheka na kutoa machozi baada ya kumuona, stori ilibadilika baada ya baba mwenye nyumba kuanza kumfokea mkewe huku akisema anawapa watoto kazi ambazo sio saizi yao.
Alipoinua mkono kumpiga mkewe na yeye kicheko kikamzidi ambapo kwa mujibu wa huyo mpishi kisa kizima kiliana kuwa kama movie na ikabidi waombe msaada kwa majirani ili kuelewa kilichotokea.
Baadhi ya majirani walifikiri kwamba huenda kuna majini yameipata hiyo familia ila wengine wakasisitiza hao watu wapelekwe kwenye kituo cha afya ambapo baada ya kupimwa damu zao zilikutwa zimejaa sumu ya dawa za kulevya, walitibiwa na kurudi nyumbani ila baba mwenye nyumba anakabiliwa na mashitaka ya kulima bangi shambani kwake.

No comments:

Post a Comment