Saturday, June 16, 2012


.
Mchezaji wa Chelsea Fernando Torres jana ameifungia timu yake ya taifa ya Hispania magoli mawili kwenye mechi na Ireland ndani ya mzigo wa Euro 2012.
Torres amesisitiza kwamba hana noma kama kocha wa timu ya taifa atamuweka benchi kwenye mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Croatia, anasema yeyote anaweza kucheza kwa sababu kikosi kina wachezaji wakali kwa hiyo kukaa benchi sio ishu.
Torres alichezeshwa dakika chache sana kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Italy ila jana kocha alimpa muda wa kutosha ambapo alionyesha ujazo wake kwa kulifungia taifa lake magoli mawili kwenye hiyo mechi ambayo walishinda nne bila ushindi ambao umeiweka Hispania kileleni kwa kufuzu kuingia kwenye mtoano.


.
Kocha wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas amejitokeza kama mmoja wa makocha wanaogombania nafasi ya kuifundisha Tottenham baada ya club hiyo kumfukuza Harry Redknap.
Kocha huyo mreno ambae sasa hivi hana kazi toka february mwaka huu inaaminika kwamba kuna uwezekano mkubwa wa yeye kupata hiyo nafasi baada ya kupata support ya kampuni ya sky bet inayoshughulika sana na ishu za mpira ambao inasemekana jana baadhi ya wakurugenzi wa club hiyo waliwasiliana na villa boas.
Tottenham inamtafuta mrithi wa kocha Harry Redknap ambae ameifundisha club hiyo kwa miaka minne kabla ya kufukuzwa juzi jumatano, Kocha wa Everton  David Moyes na kocha wa Wigan Roberto Martinez wanatajwa pia kwamba wako kwenye hiyo list ya kumchagua mmoja wa kuifundisha tottenham, lakini pia mchezaji wa zamani wa Tottenham Jurgen Klinsmann yuko kwenye hiyo list inayotajwa na vyombo vingi vya habari.


Huyo ni Shafie Dauda

EXCLUSIVE INTERVIEW NA MTOTO WA HASSAN AFIF ANAYECHEZA TIMU MOJA NA RAUL GONZALEZ


Mchana wa leo nilibahatika kufanya mazungumzo na mtoto wa mchezaji wa zamani wa Simba, Hassan Afif, Ally Afif ambaye ni mchezaji wa klabu bingwa ya bara la Asia Al Sadd ya nchini Qatar. Ally ambaye alizaliwa nchini Qatar na kuishi kidogo nchini Tanzania kabla ya yeye na baba yake Mzee Afif kurudi tena Doha ambapo ndio hasa alianza kukuza kipaji chake mpaka alipo sasa.


Nimepata kuongea mengi na Ally endelea kufuatilia shaffihdauda.com



                     
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB (YANGA)

Kamati ya Uchaguzi ya TFF inawataarifu wadau na wapenzi wa soka kuwa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa YANGA kujaza nafasi zilizowazi za Kamati ya Utendaji unaendelea vizuri chini ya Kamati ya Uchaguzi ya YANGA.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepokea kutoka Kamati ya Uchaguzi ya YANGA nakala za fomu za maombi ya uongozi wa YANGA pamoja na nakala za vyeti vya elimu vya waombaji uongozi kama sehemu ya taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi huo wa YANGA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa baadhi ya waombaji uongozi wamewasilisha nakala za vyeti vya kuhudhuria masomo ya sekondari (Secondary School Leaving Certificate) badala ya nakala za vyeti vya kuhitimu masomo ya elimu ya sekondari (Certificate of Secondary Education).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekwisha ielekeza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kuwataka wagombea wote kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10(4) na (5) inayowataka wagombea wote kujaza Fomu Na.1 ya maombi ya uongozi na  kuambatanisha nakala ya cheti cha Elimu ya Sekondari (Certificate of Secondary Education) kama ilivyoainishwa kwenye Fomu Na.1 kipengere Na.9. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA iwashauri wagombea ambao vyeti vyao vimepotea wawasiliane na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa maandishi ili kupata ‘Statement of Examination Results’ itakayotumwa kwa Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kupitia TFF kuthibitisha kuwa wamehitimu elimu ya kidato cha nne.
Uhakiki  wa vyeti vya elimu ya sekondari vya waombaji uongozi hufanywa na NECTA na vyuo husika kwa elimu ya juu kwa chaguzi za wanachama wa TFF. Wanachama wote wa TFF wanatakiwa kuzingatia kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi.
Imetolewa na:
IDARA YA HABARI
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

SHOMARY KAPOMBE MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA 2011


TUZO ZA TASWA ZILIVYOFANA USIKU HUU DIAMOND JUBILEE

Rais wa TFF, Leodegar Tenga wa pili kulia akiwa na Jellah Mtagwa kushoto kwake


Familia ya ndondi


Wadau wa ndondi
Tedi Mapunda kulia na bosi wake 


Eiphraim Mafuru kulia


Maswahiba wa siku nyingi, Shaaban Mkongwe kulia akiwa Waziri Mahadhi


Beki wa Mtibwa Salum Swedi 'Kussi'


Kaburu kulia akikabidhi tuzo


Daud Salum 'Bruce Lee' kulia akikabidhi tuzo


Athumani Hamisi akikabidhi tuzo


Asha Baraka akikabidhi tuzo


Mafuru akikabidhi tuzo


Ridhiwani Kikwete kulia akiwa na Benny Kisaka kushoto, cheko la maana


Dioniz Malinzi kushoto akikabidhi tuzo


Kapombe akipokea tuzo ya Mwanamichezo Bora Chipukizi kutoka kwa Salim Amir


Mzee Matumla akimkabidhi Kaburu tuzo ya Emmanuel Okwi


Mwenyekiti wa RT, akimkabidhi tuzo Mwanahamisi Gaucho


Aggrey Morris kushoto akipokea tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka 


Ally Choky akikabidhi tuzo


Mafuru akipakia msosi


Kim Poulsen kulia akiwa na nani sijui


Jamal Rwambow kulia na Kaburu wakati wa maakuli


Serengeti Beer inapokolea, mambo huwa hivi...


Mzee El Maamry akimkabidhi tuzo George Tarimo


Mzee Mwinyi akimkabidhi tuzo Adolph Rishard


Mzee Mwinyi akimkabidhi tuzo Peter Tino


Mzee Mwinyi akikabidhi tuzo


Waziri Mahadhi akimpokelea tuzo marehemu baba yake, Omar Mahadhi


Kaburu akimsaidia Kapombe kupokea tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka 2011 


Juma Pinto akikabidhi tuzo


Zena Chande na swahiba zake


Shaffih Dauda kulia, Amour Hassan na Michael Maluwe


Tullo Chambo na bosi wake


Akina nani sijui hawa


BIN ZUBEIRY kulia na Shaffih Dauda

No comments:

Post a Comment