Wednesday, June 13, 2012

Siku tatu za maombolezi ya Saitoti


Kenya imetangaza siku tatu za maombolezi baada ya kifo cha Waziri wa Usalama wa Kenya, Profesa George Saitoti, na naibu wake, Orwa Ojode, kwenye ajali ya helikopta ya polisi katika eneo la Ngong, nje ya Nairobi.
Profesa George Saitoti
Rais Mwai Kibaki alisema kifo cha Bwana Saitoti ni msiba mkubwa kwa taifa, na serikali imetangaza kuwa baraza la mawaziri litakutana Jumatatu, kujadili tukio hilo.
Idara ya polisi imesema uchunguzi utafanywa kujua sababu ya ajali hiyo, na balozi wa Marekani mjini Nairobi, amesema Marekani iko tayari kusaidia kwenye uchunguzi huo, ikiwa itatakiwa kufanya hivo.
Msemaji wa polisi alieleza kwamba inavoelekea kuanguka kwa helikopta hiyo lilikuwa tukio la ajali.
Raia wa Kenya walikuwa na masikitiko Jumapili, baada ya taarifa ya ajali hiyo kujulikana, na watu wamekuwa wakizuru nyumba ya kuhifadhi maiti mjini Nairobi kutoa heshima zao.
Makamo wa rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka, alipofika kwenye tukio la ajali alitoa rambi-rambi zake na alieleza wale waliokuwamo ndani ya ndege ambao wote wameteketea:
"Ndege hiyo ya aina ya Eurocopter ya police airwing, ambayo ilikuwa inaelekea Yugis, ilikuwa imembeba Waziri George Saitoti, naibu waziri Orwa Ojode na maafisa rubani wa ndege, Nancy Gitwanja na Luke Oyugi, na vilevile askari wawili ambao wanakuwa wanaandamana na Waziri Saitoti, Inspector Tonkei na Thomas Murimi"
Rambi-rambi zimekuwa zikimiminika nchini Kenya, pamoja na za Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, ambaye alipatanisha baada ya ghasia za uchaguzi uliopita nchini kenya.
Profesa Saitoti alikuwa akizungumza kwa ukali dhidi ya al-Shabaab na inaaminiwa alihusika na uamuzi wa jeshi la Kenya kuingia Somalia mwaka jana.
Bwana Saitoti aliwahi kuwa makamo wa rais na waziri wa fedha katika serikali ya Rais Moi, na akitarajiwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Alikuwa na umri wa mika 67
 

BAISKELI ZINAVYORAHISISHA MAISHA YA WANAWAKE WILAYANI RUFIJI

 Mwananmke akiendesha baiskeli kwa mkono mmoja akitoka kununua nazi sokoni mjini Utete, Rufiji
 Akina mama wakitumia baiskeli kwenda kutafuta riziki katikamji wa Ikwiriri Rufiji, mkoani Pwani jana. Picha zote na Kamanda Mwaikenda


 

SASA IKWIRIRI IKO SHWARI BAADA YA KASHESHE KUMALIZIKA

Mji wa Ikwiriri, wilayani Rufiji, Pwani, ukiwa shwari baada ya sakata la mapigano ya wakulima na wafugaji lililosababishwa na Polisi na hatimaye kumalizika hivi karibuni. Watu kadhaa walipoteza maisha katika sakata hilo. PICHA NA KAMANDA MWAIKENDA
 

Ajali ya nyingine ya magari  kati ya Rav 4 na Fusso yatokea Mbeya. 

Gari la Fusso lililo sababisha Ajali hiyo
Namba za gari la Fusso
Toyota Rav 4 ikiwa imebamizwa vibaya na Fusso hilo
Gari la Rav 4 lilivyo haribika kwa nyuma
Namba za Gari la Rav 4
Fusso kwa nyuma
Fusso kwa Mbele

***********************************
Ajali Mbaya imetokea usiku huu iiyo husisha Gari la Fusso namba T 596 BUB pamoja na Rav 4 namba
T 675 ATK, Maeneo ya CCM Mkoani Mbeya.
Shahidi aliye kuwepo eneo la tukio amedai ya kuwa Dereva wa Gari la mizigo Fusso alikuwa mwendo kasi sana, na huku akijaribu kuyapita magari mengine matano ambayo yalikuwa mbele yake. Wakati huo anaendelea kuyapita magari hayo tayali dereva wa Rav 4 alikuwa amesha washa taa kuonesha kuwa anaelekea kulia na ndipo Dereva wa fusso akaligonga Gari la Rav 4 ambalo baada ya hapo liliseleleka kwa umbali wa Takribani mita 300 kutoka usawa wa sehemu ambapo liligongewa.
Hata hivyo dereva wa Fusso aliyesababisha Ajali hiyo amekimbia eneo hilo. Hakuna aliye umia wala kupata majeruhi.
 

JK AWAAPISHA MABALOZI 10

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha mabalozi wapya kumi ambao wataongoza idara na kurugenzi mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pichani Rais akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kutoka kushoto walisimama mstari wa mbele ni Balozi Bertha Semu Somi,Balozi Hassan Simba Yahya, Balozi Vincent Joel Thomas Kibwana,Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz,Balozi Irene Mkwawa Kasyanju na Balozi Dora Mmari Msechu.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi Silima Kombo Haji,Balozi Celestine Joseph Mushy, Balozi Mbelwa Brighton Kairuki na Balozi Ramadhan Muombwa Haji(picha na Freddy Maro)

  

Rais Dkt.Jakaya Kikwete ashiriki kumuaga Muasisi wa CHADEMA Bob Makani katika viwanja vya Karimjee leo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal pamoja na Mama Salma Kikwete leo waliungana na viongozi wa CHADEMA na viongozi wengine wa kitaifa kutoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA marehemu Bob Makani ambayepia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki kuu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.(picha zote na Freddy Maro)
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe wakati wa kuaga mwili wa Muasisi wa chama cha CHADEMA marehemu Bob Makani
Rais Dkt.Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wakibeba jeneza la marehemu Bob Makani
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za Mwisho
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiteta jambo na mjumbe wa tume ya kukusanya maoni juu ya katiba Prof.Mwesiga Baregu katika viwanja vya Karimjee leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa katika viwanja vya Karimjee kufuatia msiba wa muasisi wa Chama hicho Bob Makani

TAIFA STARS, GAMBIA ZAINGIZA MIL 124/-

 
Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, D ar es Salaam imeingiza sh. 124,038,000.
Mapato hayo yametokana na washabiki 31,122 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Washabiki 25,901 walikata tiketi za sh. 3,000.
Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 18,921,050.85 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 6,555,000), bonasi kwa Taifa Stars (sh. 15,767,542.37), waamuzi (sh. 13,372,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na mafuta ya jenereta (sh. 200,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 12,834,481, asilimia 10 ya uwanja sh. 6,417,241, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,208,620, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 12,834,481 na asilimia 45 ya TFF (sh. 28,877,583).
 

Rais Kikwete na Mama Salma Wakagua mahindi Shambani kwao kijijini Msoga

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakikagua mahindi shambani kwao kijijini Msoga,Chalinze,wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki(picha na Freddy Maro)
 

WAZIRI MKUU PINDA AFUNGUA KIWANDA CHA NYUKI KIBAHA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kiwanda cha kusindika asali cha Organic Honey katika kijiji cha Visiga mkoani Pwani kinachomilikiwa na kampuni ya Boleyn International, Juni 9, 2012.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na anyepiga makofi katikati ni Mkrurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Jack Liu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mitambo baada ya kufunguza kiwanda cha kusindika asali cha  Organic Honey katika kijiji cha Visiga  mkoani Pwani  kinachomilikiwa na Kampuni ya  Boleyn  International, Juni 9, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mku
 
 

JK AMWAPISHA KATIBU TAWALA MKOA WA RUVUMA, APOKEA KITABU CHA SIMULIZI ZA WAKWERE

Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Ruvuma Bwana Hassan Mpapi Bendeyeko akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI Dkt.Aldin Mutembei akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitabu cha kwanza cha fasihi simulizi ya jamii ya Wakwere ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa Idara ya historia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Kapepwa Tambila. Dkt.Mutembei ambaye pia ni mchapishaji na msimamizi wa tafiti za Tamaduni lugha na fasihi za makabila ya Tanzania alikabidhi pia kamusi Asisi ya Kiingereza-Kiswahili na Kiarabu(picha na Freddy Maro).
 
 

No comments:

Post a Comment